Thursday, 8 November 2012

Urusi yatarajia Obama atashirikiana zaidi

Naibu waziri mkuu  katika serikali ya Urusi amesema nchi yake inatarajia  kutokana na kuchaguliwa tena  Rais  Barack Obama wa Marekani , kiongozi huyo ataonyesha ushirikiano zaidi katika suala la mabishano kuhusu mipango ya  Marekani ya makombora ya ulinzi .
Dmitry Rogozin alisema leo kwamba Urusi inatarajia Obama atazingatia wasi wasi wa Urusi kuhusu mpango wa ulinzi  barani ulaya wa Shirika la kujihami la NATO, mpango ambao unaoongozwa na Marekani. Mabishano kuhusu mpango huo wa kinga dhidi ya makombora yamezorotesha uhusiano wa Marekani na Urusi, ambayo imekataa hakikisho lililotolewa kwamba mpango huo una lengo la kujilinda dhidi ya Iran na kusema  unaweza hatimae kutumiwa kutishia uwezo wa Kinyuklia wa Urusi. Mwezi Machi mwaka huu Rais Obama bila ya kujuwa kwamba alikuwa akisikika kupitia kipaza sauti kilichokuwa wazi, alimwambia Dmitry Medvedev aliyekuwa Rais wa Urusi wakati huo, kwamba atatoa ushirikiano zaidi katika suala hilo baada ya uchaguzi wa Novemba.
                  

0 comments:

Post a Comment