Thursday 22 November 2012

KUJIINUA KUMECHANGIA KUSHINDWA KWA MAFANIKIO YANGU

KUJIINUA KUMECHANGIA KUSHINDWA KWA MAFANIKIO YANGU ‘Baada ya kubaki sina msaada wowote maishani ndipo nilipokumbuka neon lisemalo kuwa ajiinuaye atashushwa na ajishushaye atapandishwa’ Ni kauli pekee anayoweza kuielezea maishani mwake baada ya kupita huku na kule na kusahau nyuma na kusahau kuangalia mbele, Enock Fanuel ni kijana mwenye umri wa miaka 28 kutoka nchini Kenya . Katika barua yake anasema kuwa sasa amejifunza mengi kutokana na makosa aliyoyafanya ya kujiweka sehemu ya juu asiyositahili kuwepo kabla Naitwa Enock , nasoma chuo kikuu cha kenyatta mwaka wa tatu, lengo langu la kushare na wewe wakati huu kupitia blog hii ni kukuonesha mambo ambayo niliyafanya ili wewe ambaye hujayafikiria hama ama tayari wewe uliyeanza uache mara moja yasije kukuta kama yaliyonikuta, Kipindi nipo mwaka wangu wa kwanza wa masomo watu wote walioniona katika compound ya chuo hata pale mitaa nilipopita walinifikilia kuwa ninazaliwa kwenye familia ya kifahari na familia ya kiongozi mkubwa ndani ya nchi ya Kenya. Taswira hiyo ilitokana na style yangu yam aisha nilivyojionesha mbele za watu , kujifanya nafahamu kila kitu , nilikuwa na nguo kidogo lakini jinsi nilivyozitumia kuvaa mtu ambaye hakujua angedhani kuwa nina kabati zima la nguo la kuweza kuwatosheleza wanakijiji wote., Huku nikiwadanganya wengi kuwa nafanya kazi na kampuni moja kubwa , darasani nilihakikisha nakuwa wa kwanza kuamsha mkono na kujibu maswali, Kupenda wasichana ilikuwa ni kama kunywa maji nikiwadanganya mengi huku nikiwapeleka kwenye chumba tunamoishi nikitumia kuwaonesha vitu vya room met wangu kwa kujifanya vya kwangu ‘laptops,sub-woofer na vingine vingi. Room met wangu ndani ya hostel ndiye alijua ukweli kuhusu maisha yangu kwasababu sikuwa na kitu chochote bali tuviela nilitokuwa nazo za matumizi, Hivyo katika hali ya kuonekana smart kila siku nilitumia siku nyingine kuvaa nguo za room met wangu, vifaa kama catle ya kuchemsha chai alitumia kunisaidia huku nikijifanya vyakwangu, wakati ulikuja ambapo nilibaki sina hela hata ya kununua sabuni, kalamu chakula lotion body na mahitaji mengine, na kabla sijaishiwa nilijionesha kweli kuwa nina hela na wanafunzi wenzangu waliamini wengine wakiomba niwakopeshe, niwatoe chai lakini kwa kwa maneno mengi niliwadanganya. Kumaliza siku moja bila ya kuoga pamoja na kubadilisha nguo zisizokuwa za kwangu niliiona kamadhambi ya kwanza duniani, Lakini hali ilipoanza kubadilika nilianza kukosa shule , kujihusisha na shughuli za darasani zikaanza kupungua , wasichana niliowadanganya kimapenzi nikaanza kuwaona maadui machoni pangu, Mbaya zaidi ni pale msichana mmoja jirani na tunapoishi aliponiomba catlle ili akachemshe maji kwa kudhani kuwa ilikuwa ya kwangu kutokana nilivyotumia kuwambia, Shetani mbaya alipokuwa akichemsha maji cattle ilipata kuungua ,Binti alivyonipatia taarifa hiyo nilijisikia kupungua kilogram moja mwilini kwasababu nilijua fika kitu sio cha kwangu na huyu binti hawezi kulipa, kuniomba radhi kukawa kwingi wakati huo. SIkuweza kwenda kwa mtu yeyote kwa ajili ya kujikopa kwasababu nilihisi aibu kutokana na jinsi nilivyokuwa hapo awali niliamua kukaa na maumivu yangu. Nilijaribu kumwambia ukweli Yule msichana kuwa cattle haikuwa ya kwangu siku zote lakini sikupata msaada wowote. Kuchungulia mfukoni mwangu ndo sikuwa na senti hata moja ,ndugu niliamua kuweka rehani vitu vyangu vyote mpaka nilipolipa cattle hiyo. Natumai umejifunza mengi kutokana na niliyoyafanya maishani mwangu ambayo nimekuja kuyajutia baadae, ombi ni kuwa kama ulikuwa unapanga kujiinua inua inua au una tabia kama iliyokuwa ya kwangu naomba uombe rehema kwa Bwana kwani yeye ni mwaminifu Rom 10;9 Asante By Enock Mpendwa msomaji Kama una story yoyote ambayo ungependa kushare na wengine , maisha , ushauri ,testimony, kuomba ushauri, Please tutumie barua yako kupitia Tanzaniaplus@gmail.com Au kusoma barua ambazo zinatufikia kila siku tafadhali bonyeza hapa www.tanzaniaplus.blogspot.com Ungana na zaidi ya wasomaji 5000 duniani kote kwa kutembelea website yako visit your Dear reader if you any story about your life, councel, testimony, advises or any other story, please send your email now on tanzaniaplus@gmail.com You can also read some emails that we have received by clicking hire www.tanzaniaplus.blogspot.com Join with more than 5000 people who favorite website

0 comments:

Post a Comment