Thursday, 22 November 2012
HUYU NDIYE MWAFRIKA WA KWANZA MASKINI KUSOMA NJE YA NCHI
01:14
No comments
HUYU NDIYE
MWAFRIKA WA KWANZA MASKINI KUSOMA NJE YA NCHI
Moses
Kaihura alizaliwa miaka 22 iliyopita nchini Tanzania ambaye kwa sasa ni
mwanafunzi katika chuo cha cape town nchini Afrika kusini, Katika historia yake
yam aisha ya sasa anasema kuwa kama angelikuwa ni binadamu mwenye kukata tama a
anaamini asingelifika leo hii yanayomkuta maishani , Kiufupi kama mwanafunzi wa
chuo anayo mahitaji muhimu kwake kama chakula ,pocket money kwa ajili ya
kununua vitu kama sabuni ,lotion, kuingia café na kudownload material n.k,
lakini kwake vyote hivi hakuvijua wala kuvifahamu
Endelea naye………
Jina langu
naitwa Moses Kihura nina soma hapa
katika chuo cha captown Afrika Kusini, ni mtoto wa sita katika familia ya watu
sita ya mzee baba yangu Kaihura, Tangu
nikiwa mdogo familia yetu imekuwa ni ya furaha , amani na upendo kutokana na
mapenzi tuliyoendelea kuyapata kutoka kwa wazazi wetu
Mwaka 2007
wakati nikisoma kidato cha kwanza nchi Tanzania ulikuwa ni mwaka mgumu kwa
familia ambapo tulipomteza baba kipenzi kwa kifo cha ghafla, Lakini kama kijana
niliyekuwa na maono sikukata tamaa niliendelea na masomo ili kutimiza ndoto
yangu ya kimaisha.
Ukweli ni
kwamba kipindi baba yupo hai sikuwaza wala kufikiria kuwa kuna kifo au kuhisi kuwa naweza kuwa
yatima wa mzazi mmoja Lakini namshukuru Mungu ameendelea kumwezesha mama yangu
na hashindwi kamwe.
Mwaka 2010
nikiwa kidato cha nne niliamua kukabidhi maisha yangu kwa Bwana Yesu na
kuokolewa
‘KUOKOKA
JINSI ILIVYOKUWA’
‘ Nilikuwa
katika mwaka wangu wa mwisho wa masomo ndipo niliamua kumtafuta mwalimu wa
masomo ya ziada, kiukweli alikuwa ni mwalimu kati ya walimu wachache waliobaatiwa
na kipaji cha kufundisha,Alihakikisha kabla hajaanza kufundisha anatuombea na
kutufundisha neno la Mungu, siku zilizidi kusonga na Mungu ndipo alianza
kuongea nami kuwa ninapita katika njia ya kuzimu na kunionesha mabaya
yanayonizunguka ndipo niliamua kumpokea kama mwokozi wa maisha yangu.
Mwaka 2010 mwezi wa kumi nilihitimu masomo yangu na matokeo ya mtihani yalionesha kuwa sitaweza
kuendelea na kidato cha tano kwasababu nilikuwa na points 28 tu
Nikiwa mdogo
nilipenda sana kuwa mwanasheria hivyo haikuwa rahisi sana kuona ninadumaza au
mtu yeyote anaharibu ndoto yangu ya kuwa mwanasheria , nilipomwambia juu ya
hili suala alitamani kuniua kwa kuwa yeye alipenda nisomee ualimu’ Teacher’
‘kama utaweza
kujilipia mahitaji yote unaweza kwenda saivi na ninaomba usinihusishe na kitu
chochote’ niliposikia hivyo niliumia moyoni na siku nzima nilifanya kulia
,chakula sikutamani tena. Na nikabaki sina ujanja mwingine basi ndipo
nilipomwendea tena na kumwambia kuwa basi kaka nimebadilisha kozi sasa
nitasomea utalii’tourism management’ hapo alikubali, Siku ilipofika ya kwenda
chuoni nilienda peke yangu nilipofika
ilikuwa kama bahati kwangu kukuta kuwa hata kozi ya uanasheria inatolewa chuoni
hapo, ndipo nilipoongea na mkuu wa shule kwa ajili ya kubadilisha kozi yeye
alinikubalia kwasababu walichataka ni pesa yao baasi , Baada ya hapo tulipangiwa kwenda kwenye
mazoezi ya vitendo’field’ na Mungu kweli akanitumia nikafanya vizuri, Wakati
ulipofika ndipo niliamua kumwambia kakayangu tena sasa nataka kuendelea na
masomo kwa ngazi ya diploma kwasababu tumechaguliwa nchini Afrika kusini
‘Lakini hapa sikumwambia kuwa mimi
ndo nimejipangia kuendelea na masomo bali hapo nyuma nilijifanya kuwa mkuu wa
chuo kwa kumtumia email na sms zenye ujumbe wa kujipongeza kuwa nimeshinda na
nimechaguliwa kwenda Afrika kusini, na nilazima niende nisipoenda sheria
itachukua mkondo wake, kaka yangu aliamini hivyo kuwa kweli anapokea ujumbe
kutoka kwa mkuu wa chuo’
Ndipo
tulipata usafiri wa kwenda South kwa ajili ya kuanza masomo
Mpendwa
unayesoma stori hii kwa sasa nikwambie kuwa nilipofika chuoni mambo hayakuwa
marahisi kama nilivyofikilia hapo awali, Kutokana na kaka alivyo na jukumu
kubwa la kutunza familia yake na kuhakikisha kuwa watoto wake wanakwenda shule
hatukuweza kulipia mahitaji yaliyokuwa yanahitajika chuoni pamoja na hostel kwa
kuhaidi kumalizia baada ya mda mchache
Wiki ya
kwanza ilipita , ya pili mwenzi , moja na nusu, miwili Ulipofika mwezi wa kumi
katikati pesa zote za matumizi kwa ajili ya chakula ,sabuni, mafuta vikawa
vimeniishia, Deni lililokuwa limebaki la Hostelwakaanza kudaii psa yao, Mmaisha
hayakuwa rahisi, nilibadilika na kudhoofika baada ya mda mfupi,
Lakini
namshukuru mungu kwa kunipatia uwezo wa kuongea na kila mtu kwa kujenga urafiki kila sehemu nayokuwa ,
Hivyo wakati huo kutokana na ukaribu niliokuwa na o pamoja na walinzi wa Hostel
baada ya kuona jinsi navyoshinda na njaa wakaamua kuwa wananisaidia mlo mmoja
kwa siku yaani baada ya kuwa natoka chuo. Nilijaribu sana kupiga simu nyumbani
jibu nililokuwa nikipata ni kuwa’ vumilia tukipata hela tutakutumia’ sikuweza
kudhubutu kulaumu kali hiyo kwasababu nilijua fika hali halisi jinsi ilivyo
nyumbani, Narudia kusema kuwa ulikuwa
ni wakati mgumu sana , huku darasani walimu wanatupatia kazi za kufanya kama
course work kwenda kuresearch kwa internet café pamoja na kuprint kazi hiyo
kwangu sikuweza kufanya chochote kutokana na kuwa sikuwa na senti mija mfukoni.
Lakini
katika kuumia kote huko sikuchoka kumwomba Mungu , niliendele kuhudhulia
maombi, ibada nk. Mwezi mmoja ukaisha nikiwa nimeshazoea kula mlo mmoja kwa
siku , kuoga ni nadra kwa kutegeshea aliyemaliza kuoga bafuni kwa lengo la kwenda na kuangalia kama amebakiza vipande
vipande vya sabuni, haikuwa rahisi.
Kasi ya
kuhudhulia darasani ilianza kupungua leo nipo shuleni kesho hamna , course work
za walimu ndo sifanyi kutokana na kukosa hela za kuprint., mawazo mazito kila
wakati hulu marafiki na wanafunzi wenzangu wakiniuliza maswali mengi kuhusu ni
kitu gani kinachoendelea juu ya ngu, lakini jibu nililokuwa naloa ni moja tu ‘
no problem’
Mwezi wa
kumi na moja ukaingia bila uhakika wowote wa kula , nilijaribu kupiga simu tena
na kuwambia halia halisi jinsi inavyozidi kuwa mbaya , nataka kufukuzwa hostel,
nakufa na njaa ndipo walijipigapiga mfukoni wakanitumia kiasi kidogo cha Tsh
150000/ kwa maisha ya afrika kusini ni pesa kidooooogo sana, Lakini nilijua kuwa
wamejaribu kadri ya uwezo wao , nilifahamu hali jinsi ilivyo.
Nilichoamua
ni kununua unga kwa ajili ya kupika ugall kuwa natumia ugali maji mmh..sio
rahisi wenzangu.
Nakumbuka
ilikuwa ni siku ya ijumaa tarehe 15 mwezi wa 11 nilipotoka chuoni na njaa kali
na kukuta kwenye noticeboard ya hostel yaani nje ya geti kuna karatasi ya
majina ya wanafunzi watano na la kwangu likiwemo ikisema kuwa haturuhusiwi tena
kuingia bila kulipa pesa yote ya hostel, nilipojaribu kuingia ndani niliburutwa
nje kama mwizi katikati mwa wananchi wenye asila kali.
Urafiki
wangu na Askari ulibakia katika kunisaidia simu ili kuweza kuwasiliana na
nyumbani lakini kutokana kuwa walipenda na waliheshimu kazi yao wasingeliweza
kuniruhusu kuingia ndani, sikuwa na jamaa ndani ya jiji, Lakini wazo lilokuja
kichwani mwangu liliniambia kuwa leo ni ijumaa kaniasani kuna mkesha nenda
ukaombe, Ndipo nilienda kwa maombi ya usiku mzima , niliendelea kuomba mpaka
kesho yake ambapo ukweli nilisikia sauti ikinambia kuwa usiogope wala kuwaza
tena , nilitafakali sauti hii inatoka wapi lakini moja kwa moja nilielewa kuwa
ni bwana wa Mabwana Yupo pamoja name, Na hapa alichokifanya ni kuendelea
kuwatumia askari kwa kuendelea kunisaidi mahali pa kulala kwa sharti moja kuwa
‘ Hatuwezi kukuacha ulale nje lakini unapaswa kuja mahali hapa saa tatu usiku
na kuondoka mahali hapa saa kumi kamili asubuhi’ kwasababu kwa kukuruhusu
tayari tunahatarisha kazi yetu.
Nikakumbuka
mbeleni kama wiki mbili tuna mtihani wa kumaliza semester, niliangalia juu
nilipogundua kuwa anga linaweza kuwa fupi. Huku askari wakiendelea kunisisitiza
kupiga simu nyumbani na kunitumia hela
na kunielekeza mahali palipo ubalozi wa Tanzania nchi afrika kusini kwa
ajili ya kumumrisha aliyenileta kutuma pesa haraka sana, Lakini ukweli nilijua
kuwa haingeweza kusaidia kutokana na hali niliyoijua nyumbani.
Naumia sana
, najuta sana nawaza sana kwa kufikilia ndoto yangu ,sio njia rahisi kwa mwanadamu yeyote mwenye
mwili kushinda njaa , kuingia ndani saa tatu usiku , kushikavitabu kusoma,
kuamka mapema saa kumikamili, Lakini nazidi kumshukuru Mungu kwani yeye ndiye anayeendelea
kunifanikisha wakati huu, Ni yeye ni yeye ni yeye Na ninaendelea kuamini hapa na sitashindwa
kutimiza ndoto yangu , nitashinda haijarishi napitia katika wakati mgumu , Psalms 30:5
Ushauri
wangu ni mmoja kwamba tuangalie sana kwa kuwa maamuzi sahihi ni yale
yaliyokubaliwa na wazazi wako pamoja na walezi wako. Phil 4.8
Ombi Nikiwa
bado katika wakati mgumu wa maisha wewe kama ndugu uliyeguswa na history yangu naomba ushauri
nifanye nini ili niweze kushinda
Wenu
Moses
Kaihura.
Mpendwa msomaji Kama una story yoyote ambayo ungependa
kushare na wengine , maisha , ushauri ,testimony, kuomba ushauri, Please
tutumie barua yako kupitia Tanzaniaplus@gmail.com
Au kusoma barua ambazo zinatufikia kila siku tafadhali
bonyeza hapa
Ungana na zaidi ya wasomaji 5000 duniani kote kwa kutembelea
website yako
Dear reader if you any story about your life, councel,
testimony, advises or any other story, please send your email now on tanzaniaplus@gmail.com
You can also read some emails that we have received by
clicking hire www.tanzaniaplus.blogspot.com
Join with more than 5000 people who visit your favorite
website
Try Relay: the free SMS and picture text app for iPhone.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment