Thursday, 8 November 2012

Mchezo unaomkosoa Rais wasitishwa Uganda

Maafisa wa serikali nchini Uganda wamepiga marufuku mchezo wa kuigiza unaokosoa serikali ya Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni.
Mwandishi wa mchezo huo John Ssegawa alisema kuwa baraza la vyombo vya habari liliamuru kusitishwa kwa mchezo huo hadi utakapodurusiwa.
Mchezo huo unaangazia maswala ya ufisadi na uongozi duni nchini Uganda chini ya utawala wa Museveni tangu mwaka 1986.
Mwezi jana, mtengezaji vipindi mmoja alikamatwa nchini humo kwa kuonyesha mchezo wenye mada ya mapenzi ya jinsia moja bila ya idhini na maafisa wakuu.
David Cecil hata hivyo aliachiliwa kwa dhamana na kuamrishwa kusalimisha pasi yake ya usafiri.
Alifunguliwa mashtaka ya kupuuza sheria za nchi kwa kuonyesha mchezo huo kwa jina ''The River and the Mountain,'' mchezo wa kuchekesha kuhusu mwafanyabiashara anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja alivyouawa na wafanyakazi wake mjini Kampala.
Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja haviruhusiwi nchini Uganda.
Mchezo wa ''State of the Nation'' ulitengezwa ili kwenda sambamba na sherehe za kuadhimisha miaka hamsini ya uganda kujitawala.

0 comments:

Post a Comment