Thursday 8 November 2012

Polisi kudbihti mitandao ya kijamii Uganda

Polisi nchini Uganda, wanatarajiwa kudhibiti zaidi matumizi ya mitandao ya kijamii kufuatia hofu ya kusambaa kwa habari zinazozua tisho kwa usalama.
Afisaa mkuu wa polisi nchini humo aliyasema hayo kwenye mkutano wa wakuu wa polisi kutoka kanda ya Afrika Mashariki.
Generali Kale Kayihura alitoa wito kwa polisi kuhakikisha kuwa mitandao ya kijamii haitumiki kwa njia mbaya za uhalifu au kusambaza taarifa kuhusu ugaidi.
Taarifa hii ya polisi inakuja wakati wafuasi wa upinzani nchini Uganda wanatumia sana mitandao ya kijamii kuwasiliana.
“Mitandao ya kijamii ni nzuri lakini inaweza kuwa mbaya kwa jamii kwa sababu inatuma ujumbe haraka sana .” alisema Generali Kayihura.
Kayihura alikuwa anahutubia mkutano wa wakuu wa polisi kutoka kote Afrika Mashariki pamoja na wajumbe kutoka nchini Tanzania, Sudan, Sudan Kusini, Somalia, Seychelles, Burundi, Kenya, Rwanda, Ethiopia, Eritrea na Djibouti.
"Ikiwa ni taarifa nzuri ,ni vizuri’’ alisema Kayihura, lakini ikiwa ni hatari kama mfano kuhusu vile mauaji ya kimbari , au mtu amesema uongo kama mfano kuhusu ghasia za Kayunga, basi unaelewa tisho la taarifa kama hizi na athari zake.’’ aliongeza Kayihura.
Mnamo mwaka 2009, watu 21 walifariki, katika ghasia mjini Kayunga, Uganda kufuatia taarifa kuhusu ziara tatanishi ya mfalme mmoja wa kitamaduni
Harakati mfano wa misri.
Mwaka jana, maandamano ya kisiasa yalisababisha ghasia na vurugu kiasi cha kukamatwa kwa watu kadhaa.
Maandamano ya kutembea kazini yalipangwa na kiongozi wa upinzani Kiiza Besigye ambaye aliitisha maandamano mfano ya yale yaliyofanyika nchini Misri,
“Wakati maandamano ya kutembea kazini yaliposhika kasi mwaka jana, mitandao ya kijamii ndiyo ilikuwa tu imeanza kutumika hapa nchini Uganda,’’ alisema mwandishi wa habari wa BBC Ignatius Bahizi mjini Kampala.
“Lakini kwa sababu watu wengi walikuwa hawaitumii mitandao hiyo, maandamano hayo hayakuwa na athari kubwa. Watu wanaotumia mitandao ya kijamii ni watu ambao unaweza kusema ni wa kipato cha kadri au watu wanaofanya kazi na wanaweza kumudu huduma za internet’’ anaseme Bahizi
Lakini hivi karibuni, vijana wameanza kutumia mitandao hiyo kujadili mambo ya kisiasa , wakifananisha matumizi ya mitandao hiyo kuleta magezu kama inavyofanyika katika nchi za kiarabu ambapo mitandao kama Facebook ilitumika sana kuhamasisha watu na kuwaleta pamoja kwa sababu za kisiasa..
"Kuna vijana wengi wakati huu ambao wamemaliza shule na hawana ajira na ambao sasa wanatumia sana mitandao ya kijamii” alisema Bahizi na hii ndio mojawapo ya sababu ambazo polisi wanahofia’’ alidokeza Bahizi
Matamshi ya Generali Kayihura pia yaligusia wasiwasi huo.
“Hii ni mojawapo ya mambo ambayo tunapaswa kutafakari, hawa watu kutumia vijana ambao hawana ajira kuendeleza harakati zao” alisema Generali Kayihura.
unadhani wasiwasi wa polisi una ukweli wowote au ni njama tu ya kukandamiza upinzai na uhuru wa kujieleza?

0 comments:

Post a Comment