Thursday 22 November 2012

HUYU NDIYE MWAFRIKA WA KWANZA MASKINI KUSOMA NJE YA NCHI



HUYU NDIYE MWAFRIKA WA KWANZA MASKINI KUSOMA NJE YA NCHI

Moses Kaihura alizaliwa miaka 22 iliyopita nchini Tanzania ambaye kwa sasa ni mwanafunzi katika chuo cha cape town nchini Afrika kusini, Katika historia yake yam aisha ya sasa anasema kuwa kama angelikuwa ni binadamu mwenye kukata tama a anaamini asingelifika leo hii yanayomkuta maishani , Kiufupi kama mwanafunzi wa chuo anayo mahitaji muhimu kwake kama chakula ,pocket money kwa ajili ya kununua vitu kama sabuni ,lotion, kuingia café na kudownload material n.k, lakini kwake vyote hivi hakuvijua wala kuvifahamu
         Endelea naye………

Jina langu naitwa Moses  Kihura nina soma hapa katika chuo cha captown Afrika Kusini, ni mtoto wa sita katika familia ya watu sita ya mzee baba yangu  Kaihura, Tangu nikiwa mdogo familia yetu imekuwa ni ya furaha , amani na upendo kutokana na mapenzi tuliyoendelea kuyapata kutoka kwa wazazi wetu
Mwaka 2007 wakati nikisoma kidato cha kwanza nchi Tanzania ulikuwa ni mwaka mgumu kwa familia ambapo tulipomteza baba kipenzi kwa kifo cha ghafla, Lakini kama kijana niliyekuwa na maono sikukata tamaa niliendelea na masomo ili kutimiza ndoto yangu ya kimaisha.
Ukweli ni kwamba kipindi baba yupo hai sikuwaza wala kufikiria  kuwa kuna kifo au kuhisi kuwa naweza kuwa yatima wa mzazi mmoja Lakini namshukuru Mungu ameendelea kumwezesha mama yangu na hashindwi kamwe.
Mwaka 2010 nikiwa kidato cha nne niliamua kukabidhi maisha yangu kwa Bwana Yesu na kuokolewa
‘KUOKOKA JINSI ILIVYOKUWA’
           Nilikuwa katika mwaka wangu wa mwisho wa masomo ndipo niliamua kumtafuta mwalimu wa masomo ya ziada, kiukweli alikuwa ni mwalimu kati ya walimu wachache waliobaatiwa na kipaji cha kufundisha,Alihakikisha kabla hajaanza kufundisha anatuombea na kutufundisha neno la Mungu, siku zilizidi kusonga na Mungu ndipo alianza kuongea nami kuwa ninapita katika njia ya kuzimu na kunionesha mabaya yanayonizunguka ndipo niliamua kumpokea kama mwokozi wa maisha yangu.
Mwaka 2010  mwezi wa kumi nilihitimu masomo yangu  na matokeo ya mtihani yalionesha kuwa sitaweza kuendelea na kidato cha tano kwasababu nilikuwa na points 28 tu
Nikiwa mdogo nilipenda sana kuwa mwanasheria hivyo haikuwa rahisi sana kuona ninadumaza au mtu yeyote anaharibu ndoto yangu ya kuwa mwanasheria , nilipomwambia juu ya hili suala alitamani kuniua kwa kuwa yeye alipenda nisomee ualimu’ Teacher’  
‘kama utaweza kujilipia mahitaji yote unaweza kwenda saivi na ninaomba usinihusishe na kitu chochote’ niliposikia hivyo niliumia moyoni na siku nzima nilifanya kulia ,chakula sikutamani tena. Na nikabaki sina ujanja mwingine basi ndipo nilipomwendea tena na kumwambia kuwa basi kaka nimebadilisha kozi sasa nitasomea utalii’tourism management’ hapo alikubali, Siku ilipofika ya kwenda chuoni nilienda peke yangu  nilipofika ilikuwa kama bahati kwangu kukuta kuwa hata kozi ya uanasheria inatolewa chuoni hapo, ndipo nilipoongea na mkuu wa shule kwa ajili ya kubadilisha kozi yeye alinikubalia kwasababu walichataka ni pesa yao baasi  , Baada ya hapo tulipangiwa kwenda kwenye mazoezi ya vitendo’field’ na Mungu kweli akanitumia nikafanya vizuri, Wakati ulipofika ndipo niliamua kumwambia kakayangu tena sasa nataka kuendelea na masomo kwa ngazi ya diploma kwasababu tumechaguliwa nchini Afrika kusini
            ‘Lakini hapa sikumwambia kuwa mimi ndo nimejipangia kuendelea na masomo bali hapo nyuma nilijifanya kuwa mkuu wa chuo kwa kumtumia email na sms zenye ujumbe wa kujipongeza kuwa nimeshinda na nimechaguliwa kwenda Afrika kusini, na nilazima niende nisipoenda sheria itachukua mkondo wake, kaka yangu aliamini hivyo kuwa kweli anapokea ujumbe kutoka kwa mkuu wa chuo’
Ndipo tulipata usafiri wa kwenda South kwa ajili ya kuanza masomo
Mpendwa unayesoma stori hii kwa sasa nikwambie kuwa nilipofika chuoni mambo hayakuwa marahisi kama nilivyofikilia hapo awali, Kutokana na kaka alivyo na jukumu kubwa la kutunza familia yake na kuhakikisha kuwa watoto wake wanakwenda shule hatukuweza kulipia mahitaji yaliyokuwa yanahitajika chuoni pamoja na hostel kwa kuhaidi kumalizia baada ya mda mchache
Wiki ya kwanza ilipita , ya pili mwenzi , moja na nusu, miwili Ulipofika mwezi wa kumi katikati pesa zote za matumizi kwa ajili ya chakula ,sabuni, mafuta vikawa vimeniishia, Deni lililokuwa limebaki la Hostelwakaanza kudaii psa yao, Mmaisha hayakuwa rahisi, nilibadilika na kudhoofika baada ya mda mfupi,
Lakini namshukuru mungu kwa kunipatia uwezo wa kuongea na kila mtu  kwa kujenga urafiki kila sehemu nayokuwa , Hivyo wakati huo kutokana na ukaribu niliokuwa na o pamoja na walinzi wa Hostel baada ya kuona jinsi navyoshinda na njaa wakaamua kuwa wananisaidia mlo mmoja kwa siku yaani baada ya kuwa natoka chuo. Nilijaribu sana kupiga simu nyumbani jibu nililokuwa nikipata ni kuwa’ vumilia tukipata hela tutakutumia’ sikuweza kudhubutu kulaumu kali hiyo kwasababu nilijua fika hali halisi jinsi ilivyo nyumbani,   Narudia kusema kuwa ulikuwa ni wakati mgumu sana , huku darasani walimu wanatupatia kazi za kufanya kama course work kwenda kuresearch kwa internet café pamoja na kuprint kazi hiyo kwangu sikuweza kufanya chochote kutokana na kuwa sikuwa na senti mija mfukoni.
Lakini katika kuumia kote huko sikuchoka kumwomba Mungu , niliendele kuhudhulia maombi, ibada nk. Mwezi mmoja ukaisha nikiwa nimeshazoea kula mlo mmoja kwa siku , kuoga ni nadra kwa kutegeshea aliyemaliza kuoga bafuni kwa lengo  la kwenda na kuangalia kama amebakiza vipande vipande vya sabuni, haikuwa rahisi.
Kasi ya kuhudhulia darasani ilianza kupungua leo nipo shuleni kesho hamna , course work za walimu ndo sifanyi kutokana na kukosa hela za kuprint., mawazo mazito kila wakati hulu marafiki na wanafunzi wenzangu wakiniuliza maswali mengi kuhusu ni kitu gani kinachoendelea juu ya ngu, lakini jibu nililokuwa naloa ni moja tu ‘ no problem’
Mwezi wa kumi na moja ukaingia bila uhakika wowote wa kula , nilijaribu kupiga simu tena na kuwambia halia halisi jinsi inavyozidi kuwa mbaya , nataka kufukuzwa hostel, nakufa na njaa ndipo walijipigapiga mfukoni wakanitumia kiasi kidogo cha Tsh 150000/ kwa maisha ya afrika kusini ni pesa kidooooogo sana, Lakini nilijua kuwa wamejaribu kadri ya uwezo wao , nilifahamu hali jinsi ilivyo.
Nilichoamua ni kununua unga kwa ajili ya kupika ugall kuwa natumia ugali maji mmh..sio rahisi wenzangu.
Nakumbuka ilikuwa ni siku ya ijumaa tarehe 15 mwezi wa 11 nilipotoka chuoni na njaa kali na kukuta kwenye noticeboard ya hostel yaani nje ya geti kuna karatasi ya majina ya wanafunzi watano na la kwangu likiwemo ikisema kuwa haturuhusiwi tena kuingia bila kulipa pesa yote ya hostel, nilipojaribu kuingia ndani niliburutwa nje kama mwizi katikati mwa wananchi wenye asila kali.
Urafiki wangu na Askari ulibakia katika kunisaidia simu ili kuweza kuwasiliana na nyumbani lakini kutokana kuwa walipenda na waliheshimu kazi yao wasingeliweza kuniruhusu kuingia ndani, sikuwa na jamaa ndani ya jiji, Lakini wazo lilokuja kichwani mwangu liliniambia kuwa leo ni ijumaa kaniasani kuna mkesha nenda ukaombe, Ndipo nilienda kwa maombi ya usiku mzima , niliendelea kuomba mpaka kesho yake ambapo ukweli nilisikia sauti ikinambia kuwa usiogope wala kuwaza tena , nilitafakali sauti hii inatoka wapi lakini moja kwa moja nilielewa kuwa ni bwana wa Mabwana Yupo pamoja name, Na hapa alichokifanya ni kuendelea kuwatumia askari kwa kuendelea kunisaidi mahali pa kulala kwa sharti moja kuwa ‘ Hatuwezi kukuacha ulale nje lakini unapaswa kuja mahali hapa saa tatu usiku na kuondoka mahali hapa saa kumi kamili asubuhi’ kwasababu kwa kukuruhusu tayari tunahatarisha kazi yetu. 
Nikakumbuka mbeleni kama wiki mbili tuna mtihani wa kumaliza semester, niliangalia juu nilipogundua kuwa anga linaweza kuwa fupi. Huku askari wakiendelea kunisisitiza kupiga simu nyumbani na kunitumia hela  na kunielekeza mahali palipo ubalozi wa Tanzania nchi afrika kusini kwa ajili ya kumumrisha aliyenileta kutuma pesa haraka sana, Lakini ukweli nilijua kuwa haingeweza kusaidia kutokana na hali niliyoijua nyumbani.
Naumia sana , najuta sana nawaza sana kwa kufikilia ndoto yangu  ,sio njia rahisi kwa mwanadamu yeyote mwenye mwili kushinda njaa , kuingia ndani saa tatu usiku , kushikavitabu kusoma, kuamka mapema saa kumikamili, Lakini nazidi kumshukuru Mungu kwani yeye ndiye anayeendelea kunifanikisha wakati huu, Ni yeye ni yeye ni yeye  Na ninaendelea kuamini hapa na sitashindwa kutimiza ndoto yangu , nitashinda haijarishi napitia katika wakati mgumu , Psalms 30:5
Ushauri wangu ni mmoja kwamba tuangalie sana kwa kuwa maamuzi sahihi ni yale yaliyokubaliwa na wazazi wako pamoja na walezi wako.  Phil 4.8
Ombi Nikiwa bado katika wakati mgumu wa maisha wewe kama ndugu  uliyeguswa na history yangu naomba ushauri nifanye nini ili niweze kushinda
Wenu
Moses Kaihura.


Mpendwa msomaji Kama una story yoyote ambayo ungependa kushare na wengine , maisha , ushauri ,testimony, kuomba ushauri, Please tutumie  barua yako kupitia  Tanzaniaplus@gmail.com
Au kusoma barua ambazo zinatufikia kila siku tafadhali bonyeza hapa
Ungana na zaidi ya wasomaji 5000 duniani kote kwa kutembelea website yako

Dear reader if you any story about your life, councel, testimony, advises or any other story, please send your email now on tanzaniaplus@gmail.com
You can also read some emails that we have received by clicking hire www.tanzaniaplus.blogspot.com
Join with more than 5000 people who visit your favorite website




Try Relay: the free SMS and picture text app for iPhone.

0 comments:

Post a Comment