Thursday, 27 September 2012

TUJIULIZE WENYEWE KWANZA

TUJIULIZE WENYEWE KWANZA


MASWALI YA KUJIULIZA WEWE MWENYEWE BINAFSI

Muda mwingi huwa tunapenda kuwauliza watu wengine maswali.Lakini mimi nitakuwa nakuletea maswalimatano yakujiuliza wewe mwenyewe binafsi.
1.Wewe ni nani?
2.Unajipenda?kama ndio kwa nini kama sio kwa nini?
3.Ni vitu gani muhimu katika maisha yako?
4.Ni mafanikio gani unayojivunia katika maisha yako kwa sasa?
5.Nini lengo lako duniani?kwa nini upo duniani?

Kwa leo maswali matano ni hayo na nitakuwa nakuwekea mara kwa mara.Sio lazima unijibu mimi,jijibu wewe mwenyewe ila unaweza kushare nami kunifahamisha kama umeguswa.

NOTE:Kama ni mtu wa kuchukua mambo kirahisi bila kufikiri kwa kina unaweza kuhisi ni maswali yasiyo na maana.Ila ni maswali makubwa sana unayotakiwa kujiuliza.

0 comments:

Post a Comment