Friday, 18 January 2013

Moto wazidi kuiangamiza nchi ya Australia

Raia kadhaa wa Australia wamepoteza makaazi yao leo wakati joto linalozidi kupanda liliposababisha moto mpya wa msituni kusini-mashariki mwa nchi hiyo, na kuchochea mwingine ambao vikosi vya zima moto vilidhani vimefanikiwa kuudhibiti. Jiji la Sydney limeshuhudia siku ya joto kali zaidi kwa kuwa na nyuzi joto 45.8, huku  hospitali zikipokea idadi kubwa ya wagonjwa waliokabiliwa na shinikizo lilitokana na joto hilo. Kitongoji cha Victoria katika jimbo la Licola, kilomita 240 mashariki mwa Melbourne kilizingirwa na moto kabisa na wakaazi 10 waliokuwa wamebakia huko waliambiwa kutafuta hifadhi kwa namna yoyote wanayoweza. Mamlaka ya zima moto nchini Australia imesema nyumba zisizopungua tano katika vijiji vya Seaton na Heyfield zimeteketea kwa moto.

0 comments:

Post a Comment