This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Saturday 26 January 2013

Why Me God Video

Why Me, God?

Why Me, God? - A Common Question
I'm sure you are asking, "Why me, God?" because something has happened that caused you to feel somehow singled out. Perhaps you feel that God must be punishing you for some reason. Why else would this be happening to you? Be assured. You are not alone. God has not abandoned you and He has not singled you out, no matter how you feel right now. Whatever you are going through, God's promise is that He will see you through and give you the strength and direction you need. God wants you to know that He understands how you feel, that He knows more about your situation than you do, and that He saw it coming before you did. Above all, He began to work on His resolution for you before you even knew to ask! The reality here is that God is for you. He is not against you.
Why Me, God? - An Erred Belief System
Our feelings of "Why me, God?" are real. They are based on real events, but our conclusions may not be accurate. While we don't want to minimize the pain you feel in any way, we do want to try to help you look more closely at why you feel singled out and whether or not you've arrived at a valid conclusion. The answers to why we conclude anything, even why we question God's intent or purpose in any event, can be found in our highly individualized network of beliefs.

We absorb our beliefs from our parents, teachers, life experiences, books, etc. Some of what we have come to believe may sound right, but in reality our views might be too narrowly defined or inaccurate. We have bought into many ideas and concepts that distort our right thinking and actually work against us. For example, we have learned untruths that cause us to live the role of the victim, either of circumstances or of our past. These erred beliefs cause us to cry out in pain, "Why me, Lord?"

God's answer is that we are not victims but victors. God has said that we can trust Him in everything and that every event in our lives should be counted as ALL joy (James 1:2). He has also told us that He will cause good to come out of every situation for those who love Him (Romans 8:28). When we ask "Why me, God" it's really because we don't believe God. Our belief system opposes God, so we feel singled out and victimized.

Most of us believe, at least on some level, that we need to understand everything. We just need to know why. When we don't, we may feel God has betrayed us in some way. In reality, it's not God who is confusing us or betraying us, it is our belief system. All those inconsistent, partially correct beliefs cause us to question God's fairness in what we are experiencing. For example, somewhere in our belief system, we may have come to believe that we deserve to be blessed because we have been diligent to honor God, been a good person, fed the hungry, or helped our neighbor. We often believe that the things we do should keep us from harm's way. Then when something bad happens, we are confused and ask God why.
Why Me, God? - Changing our Thinking
When something happens that deeply touches us, we often ask, "Why me, God?" We are quick to judge the event as good or bad. What if we were to eliminate the possibility that anything that happens to us is inherently bad and choose to believe that everything that happens to us is always good? Impossible, you say? It has to be one or the other, doesn't it?

Belief systems are changeable. When we discover that something we have believed, even for a long time, is no longer valid, can we not simply change our mind and fully embrace the new? If you are crying out "Why me, God?" you must believe there is a God out there who hears you and you have hoped He would answer you. Maybe there was a time when you didn't believe there was a God at all. If you changed your mind and opened your life to God, then you can also change your mind about judging events as being bad for you.

When we choose to believe that ALL the events in our life are good for us, even the ones that seem frustrating and painful for now, we are agreeing with God! When we choose to believe and trust God that there will always be a good outcome, we are trusting Him! Only God knows why we are going through these circumstances. Our new dialogue with God will be, "God, this is going to be an interesting journey. I'm excited to see how you are going to bring good out of this one. I trust you will!"

Saturday 19 January 2013

When I think about Gods Love, I told my heart to not leave your servior

 Nine people have died instantly in the Road accident, that occured late today in Bukoba town Tanzania
 So what I want to mean, because all of us we know its accident, and it occurs ussually many people loose their life, but where are they going after dying, and its my hope that today you have used vehicle but you arrive saftely, so know that Jesus waiting with open hand to surrender your life.

My dear just ask your self why not you, do you think this guys did wrong than you, if not just decide to recieve Jesus today

Friday 18 January 2013

Double life

UTANGULIZI Mwandishi mmoja alimwuliza Bwana Yesu: Katika amri zote ni ipi iliyo kuu? (Mk. 12:28). Bwana alimjibu: Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. (Mk. 12:29-30). Hicho ndicho kipimo cha utimilifu wa utii. Tunapoamua kumfuata Yesu, hata hivyo, hatukamiliki kwa siku moja. Maisha ya wokovu ni safari; ni mchakato wa kukua kuanzia uchanga, utu uzima, hadi utimilifu wa Kristo. (1 Pt. 2:2; Ebr. 5:12-14). Mabadiliko ya ukuaji wetu kiroho hayafanyiki kwa juhudi zetu wenyewe – ni Roho Mtakatifu ndiye anayetubadilisha. Wajibu wetu ni kumpa nafasi ili aweze kufanya hivyo. Hiyo ni kusema kwamba, kazi ya Roho Mtakatifu ndani yetu inategemea mwenendo wetu na kiwango kile cha utayari tulio nao wa kutii neno lake; na pia bidii na shauku yetu ya kumtafuta Bwana. Yeye anasema: Nawapenda wale wanipendao na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. (Mith. 8:17). KABLA YA KUOKOLEWA Kabla ya kuokolewa tunakuwa ni watu wa duniani. Mawazo, maneno, na matendo yetu yanakuwa ni ya kidunia; maana dunia ina kawaida zake ambazo ni tofauti kabisa na zile za kimbingu. Maandiko yanasema: Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu. (1 Kor. 6:9-11). Vilevile imeandikwa: Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo ... (Gal. 5:19-21). Huko ndiko ambako tunakuwa kabla ya kuamua kumpokea Yesu mioyoni mwetu na kumwachia utawala wa maisha yetu. Wakati tungali kule, maandiko yanasema: Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nao tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine. (Efe. 2:1-3). BAADA YA KUOKOLEWA Bwana alipowaokoa wana wa Israeli, hakuwaacha wabakie palepale Misri. Aliwaambia wajiandae kuondoka ili awapeleke katika nchi ya Kanaani. Hali kadhalika, Bwana anapotuokoa, anataka tutoke duniani na kuingia kwenye ufalme mpya wa Kristo. Imeandikwa: Kwa hiyo, Tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana, msiguse kitu kilicho kichafu, nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi. (1 Kor. 6:17-18). Japokuwa bado tunaendelea kubaki hapahapa duniani, maandiko yanasema: Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake. (Wakolosai 1:13). Ukiokolewa unakuwa umeingizwa katika ufalme wa Kristo; na jambo hili ni halisi kabisa katika ulimwengu wa roho! Wana wa ulimwengu wana tabia na mwenendo wao unaowatambulisha. Hali kadhalika wana wa Mungu nao wanatambulishwa na tabia na mwenendo tofauti na ule wa dunia. Unapoona kwamba mwana wa Mungu ana tabia za kidunia, basi hapo liko tatizo ambalo mhusika anatakiwa kuchukua hatua haraka iwezekanavyo. Bwana anasema sasa: Kama watoto wenye kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. (1 Petro 1:14-16). Kuwa watakatifu maana yake nini? Ni kuwa tofauti kabisa na dunia na kuwa sawasawa na Mungu. Imeandikwa: Msiipende dunia wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. (1Yoh. 2:15- 16). MAISHA YA AINA MBILI Hebu tujiulize maswali yafuatayo. Kama Mungu anasema kwamba tutoke kati ya dunia; pia tusiipende dunia na mambo yake; je, tuseme nini juu ya mtu mwenye hali hizi: Akiwa kanisani ni mtu mnyenyekevu lakini akiwa nje ni mkali na mgomvi. Jumapili anavaa kwa heshima lakini siku zingine anavaa mavazi ya kidunia (yaani yale ambayo hata yeye mwenyewe anayaonea aibu kuyavaa kanisani). Jumapili anasikiliza muziki wa injili lakini siku zingine ni muziki wa kidunia. Simu yake ina nyimbo za injili na taarabu za mipasho. Anahudhuria matamasha ya Kikristo na matamasha ya muziki wa kidunia; au hata disko na klabu za usiku. Kanisani anatoa sadaka lakini ofisini anaandika risiti za uongo ili apate malipo zaidi ambayo si haki yake. Mbele za wapendwa anaongea maneno ya Mungu lakini mbali nao amejaa mizaha na maneno ambayo mbele ya wapendwa hana ujasiri wa kuyatamka. Kanisani anaonekana mkamilifu lakini akiwa nje anaangalia picha za ngono; na hata kwenye simu yake anazo. Unadhani Mungu anaposema, “Msiipende dunia wala mambo yaliyomo katika dunia”, mambo hayo ni yapi? Je, ni tofauti na hayo tuliyoyaona hapo juu ambayo yanatendeka nje ya kanisa? Ni wazi kwamba ndiyo hayohayo. Kama Mungu anasema: “Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake”, je, unatambua kwamba mtu kusema tu kwamba “mimi ni Mkristo” lakini bado akawa anayatenda hayo kunabatilisha kabisa ukristo wake? Kumkataa Mungu si lazima mpaka mtu atamke hivyo waziwazi. Wengi wanajiita Wakristo lakini kwa kitendo cha kuipenda dunia, Mungu anasema, kumpenda Baba hakumo ndani yao. HASARA YA MAISHA MAWILI Kwa nini ufanye kazi yenye hasara? Kwa nini uende kanisani maisha yako yote, kisha mwisho wake uje ukataliwe? Bwana anasema: Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani, lakini akisitasita, roho yangu haina furaha naye. (Ebr. 10:38). Kusitasita maana yake ni kuingia kanisani, lakini hutaki kubaki kwa Mungu asilimia mia moja. Badala yake kanisani umo nusu na duniani umo nusu. Pia imeandikwa: Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala hu moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. (Ufu. 3:16-16). Mtu aliye uvuguvugu hahesabiwi miongoni mwa wana wa Mungu! Vilevile Bwana anasema: Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyotenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilokosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa. (Yer. 18:24). Wako watu wengi ambao, katika maisha yao yote wanadhani kuwa wako ndani ya Mungu, lakini siku ya mwisho itakuwa ni masikitiko makubwa. Watajikuta wakikataliwa kwa vile walikuwa wakiishi maisha mawili – upande mmoja wanamkubali Mungu; upande wa pili bado wameshikilia kawaida za dunia. NINI CHA KUFANYA? Bwana anataka tuwe na msimamo na kuchagua upande mmoja tu. Maandiko yanasema wazi kuwa: ....nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako. (Kumb. 30:19). Kupotea ni ama mtu ameamua kwa makusudi kutomtii Mungu au hakutafuta maarifa ya Mungu. Makwazo unayokutana nayo hayapo hapo kwa bahati mbaya. Bwana anaruhusu yakufike ili uweze kuchagua kati ya kumtii yeye au kufuata mawazo ya adui. Yafuatayo ni maandiko ambayo yanatupa maarifa au maelekezo ya nini cha kufanya ili tusiwe watu wenye maisha mawili ambayo mwisho wake ni kukataliwa: Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya mto, ....lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA. (Yoshua 24:15). Ni vema kuchagua kumtumikia Bwana. Usianze kutoa visingizio kwamba, “Unajua maisha ni magumu, ndiyo maana ninafanya hivi.” Sababu hizo hazitakusaidia mwisho wa safari. Chagua kusimama na Bwana naye atashughulikia mambo yako. Usiwe na mawe ya kupimia mbalimbali, kubwa na dogo, katika mfuko wako. Usiwe na vipimo mbalimbali, kikubwa na kidogo, katika nyumba yako. Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako. Kwa kuwa wote wayatendao mambo kama haya, wote watendao yasiyo haki, ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako. (Kumb. 25:13-16). Hapa hazungumzii tu wafanyabiashara, bali anazungumzia suala la viwango. Usipunguze viwango viwe vya kimwili au vya kiroho. Usipime mambo, upande mmoja kwa mtazamo wa kimungu na upande mwingine wa kidunia. Jiwe timilifu la haki ni Neno la Kristo. Kama neno linasema ‘fanya hivi’, basi hicho ndicho cha kufanya hata kama dunia yote iko kinyume nacho. Macho yako yatazame mbele, na kope zako zitazame mbele yako sawasawa. Ulisawazishe pito la mguu wako, na njia zako zote zithibitike. (Mith. 4:25-26). Chagua upande wa Mungu na uwe thabiti ndani yake badala ya kuyumbayumba – mara duniani, mara kwa Mungu. Msiipende dunia wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. (1Yoh. 2:15- 16). Maadamu tungali duniani, tutakabiliana na tamaa na misukumo mbalimbali yenye nguvu kutoka kwa marafiki, ndugu, hali ya uchumi, wafanyakazi wenzetu, nk. Lakini, tunalazimika kukataa kuvutwa na mambo ya dunia yaliyo kinyume na neno la Mungu hata kama yanaonekana ni ya kisasa; na hata kama sisi tutaitwa tumepitwa na wakati. Kuna faida kumpenda Mungu kuliko kuipenda dunia ambayo ni ya muda mfupi tu. Mungu wetu ni wa milele yote! HITIMISHO Usipofanya uamuzi, usidhani kwamba Mungu atakulazimisha. Watu wengi hupenda kusema kwamba, “Mungu anisaidie niache hiki au kile ...”. Maandiko yanasema: Asiyetawala roho yake ni mfano wa mji uliobomolewa usio na kuta. (Mith. 25:26). Maana yake ni kuwa, adui shetani anaingia na kutoka apendavyo katika moyo wa aina hiyo; anaingiza takataka zake kama apendavyo na kukuwekea mawazo ya uongo. Mathalani mtu anapofanya mambo mbalimbali anaweza kujitetea kwa kusema: nasikiliza muziki wa kiduania ili kutuliza mawazo na kujiburudisha; nasikiliza muziki wa kidunia ili kujipatia mafunzo mbalimbali; naenda kwenye klabu ili kujumuika na marafiki na kupeana mawazo, n.k. Sababu kama hizo zinaonekana ni nzuri lakini ukweli ni kwamba yote hayo ni uongo wa kuzimu ambao mwisho wake ni upotevu na uangamivu! Kumbuka shetani haji kama shetani, bali huja kama malaika wa nuru. (2 Kor. 11:14). Kwanza ni lazima uamue kuacha na kisha uanze kuacha; kisha Mungu atakushika mkono kuanzia hapo. Israeli walipofika baharini huku Wamisri wakiwa wanakuja nyuma yao, Bwana alimwambia Musa: Mbona unanililia mimi? Waambie wana wa Israeli waendelee mbele. Nawe inua fimbo yako, ukanyoshe mkono wako juu ya bahari, na kuigawanya; nao wana wa Israeli watapita kati ya bahari katika nchi kavu. (Kut. 14:15-16). Kugawanyika kwa bahari kulifuatia hatua yao ya imani ya kusonga mbele wakati bahari ingali imejaa. Ilikuwa ni vivyo hivyo pale walipofika kwenye mto Yordani wakiwa na Yoshua. Makuhani walitakiwa kuyakanyaga maji kwanza ndipo maji yalitindika. (Yoshua 3:15-16). Kwa hiyo, Mungu anasema: Usiandamane na mkutano kutenda uovu. (Kut. 23:2). Yaani, usifanye mambo kwa kisingizio cha kusema kwamba, “Mbona kila mtu anafanya hivyo?” Kama Mungu akizuia jambo, kubali hata kubaki peke yako katika kumtii Mungu. Wacha dunia yote ielekee upande wake lakini wewe amua kusimama na Bwana hadi mwisho! Bwana anasema: Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu. (2 Yoh. 1:8). Pia anasema: Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. (Ufu. 3:11). Inawezekana! Unaweza! Amua leo na kusimama na Bwana!

jE KUNA ULINZI WOWOTE KUTOKA KWA IBIRISI

Ulinzi Kutoka kwa Waganga wa Kienyeji Naamini umeshasikia mara kadhaa watu wakitaja kile kinachoitwa “sayansi ya kiafrika”. Kwa kifupi maneno haya yanaongelea kazi za waganga wa kienyeji. Ni wazi kuwa yanamaanisha upigaji ramli, uaguzi, usafishaji nyota, na hata ulozi na mengine kama hayo. Siku hizi watu wengi wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji kwa lengo la kupata “mafanikio”, wakiwamo wanasiasa, wafanyabiashara, wafanyakazi, wake, waume, wapenzi, wachumba, wanamuziki, na hata wale wanaotaka kuwakomesha wabaya wao. Ukipita sehemu nyingi, utakutana na matangazo ambayo, japo yanashangaza, lakini watu wanaenda kwa hao walioyaweka! Kumfunga mpenzi mkorofi, kuzindika nyumba, kusafisha nyota, kupata kazi, n.k. ni baadhi ya maneno yaliyo kwenye mabango hayo. Kilichonishangaza mimi ni kuwa, kuna hata matangazo yanayosema wazi kabisa “Njoo tukusaidie kupata utajiri wa majini”!! Sisemi kuwa hakuna dawa za kienyeji. La hasha! Zipo nyingi na nzuri kabisa. Lakini linapofikia suala la kuaguana na kuambiana kutumia dawa huku mtu yuko uchi, au aangalie mashariki, au akanywee makaburini, n.k., hapo liko jambo. Kabla sijamjua Yesu, niliwahi kwenda kwa mganga mmoja. Alinipa dawa kwenye kichupa kidogo. Na akanipa sharti la kwenda kuinywa usiku wakati watu wote wamelala; na nihakikishe hanioni mtu yeyote. Lakini kabla ya kuondoka kwake, alinichanja chale, ambapo aliniambia nifumbe macho na nisifungue kabisa wakati anaponichanja! Haya ni mambo ambayo yanafanyika kila siku sehemu mbalimbali. Alikuwapo mfalme mmoja wa Israeli aliyeitwa Sauli, ambaye alimwasi BWANA. Baada ya kuona mambo hayamwendei vema, siku moja aliwaambia watumishi wake: Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. (1 Samweli 28:7). Alipofika kwa huyo mwanamke, akamwambia: Tafadhali nibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako.... Nipandishie Samweli. (1 Sam 28:8, 11). Samweli alikuwa ni nabii mkubwa wa Mungu ambaye kwa wakati huo alishakufa. Kwa hiyo, kwa kutojua kwake, Sauli akataka eti apandishiwe huyo nabii kutoka huko aliko apate kuomba msaada kwake ili mambo yake ya kiutawala yamnyokee. Hatimaye, huyo mwanamke mtabiri alipopiga manyanga yake na kuzama kwenye ulimwengu wa roho, akasema: Naona mungu anatoka katika nchi. Sauli akainama mpaka nchi, akasujudia. (1 Sam 28:13-14). Ukweli ni kuwa huyo aliyeonekana hakuwa Mungu wala Samweli. Ndivyo ilivyo hata leo. Ukienda kwa mpiga ramli atafanya mambo yake, kisha ataondoka katika ufahamu wa kawaida wa kibinadamu ili aweze kuwasiliana na viumbe wa rohoni. Sasa ni kitu gani hasa kinachoendelea hapa? Ulimwengu huu unaongozwa na nguvu zisizoonekana. Zipo nguvu za aina mbili kuu – kuna nguvu za nuru na nguvu za giza. Niseme tu kuwa hakuna kitu kama “sayansi ya kiafrika”, bali ni matumizi ya mapepo/majini/mashetani. Hawa ni viumbe halisi kabisa, lakini ni wenye akili na nguvu kuliko mwanadamu. Yule aliyeonwa na mwanamke ambaye mfalme Sauli alimwendea alikuwa ni pepo wa kutoka kuzimu. Mungu hatoki katika nchi; anatoka mbinguni! Ndivyo watu wanavyodanganywa hata leo hii. Wanasema wanaongea na babu au bibi zao waliokufa. Ukweli ni kuwa huyo anakuwa ni pepo kabisa. Anapokuja, anakutaka labda ufanye mambo ya uganga, n.k. Ni pepo; ni jini; ni shetani! Au wale wanaoenda kutambika kwenye makaburi wakidhani wanaongea na wazee wao. Ndugu, hapo unafanya biashara na mashetani kabisa! Biblia inasema: Kwa kuwa liko tumaini kwa yule aliyeambatana na wote walio hai; (maana ni afadhali mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa); kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui lolote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. (Mhubiri 9:4-5). Tapeli anapokuja kwako kwa maneno matamu, laini, ya kuvutia, utafurahi na kudhani umepata rafiki. Lakini nia yake ni kukumaliza. Unaweza hata kunywa soda yake tamu, halafu kesho yake ukajikuta uko mtaroni, hujitambui, na umeibiwa kila kitu. Majini ni viumbe wenye hila. Hata kama wanachofanya kinaonekana kizuri, mwisho wake ni uangamivu. Maana kama ni “kufanikiwa”, utafanikiwa kabisa. Maandiko yanasema: Wala si ajabu, maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. (2 Wakorintho 11:14). Lakini Bwana Yesu anatupa hali halisi ilivyo kuhusiana na Shetani na mapepo yake. Anasema: mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu. (Yohana 10:10). Shetani ni mwizi, mharibifu na mwuaji tu. Hana pungufu au zaidi ya hapo! Akikupa kitu , hata iwe ni utajiri wa mabilioni, ni kwa lengo moja tu; kukuangamiza! Mungu anasemaje kuhusu hii ‘sayansi ya kiafrika’? Naamini umeshasikia mara nyingi watu wakisema, “Jisaidie na Mungu naye atakusaidia.” Siwezi kukataa lakini kama ni Mungu huyu ninayekuambia habari zake hapa, Yeye anasema kinyume kabisa cha hayo. Imeandikwa: Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako. (Mithali 3:5-6). Sasa watu wengi wanasema kuwa kwenda kwa waganga ni katika jitihada hizo za kujisaidia. Bwana wa majeshi anasema hivi: Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute, ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. (Mambo ya Walawi 19:31) Na anaonya kwa ukali kabisa kuwa: Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake. (Mambo ya Walawi 20:6). Kuzini inaweza kumaanisha maana hii ya kawaida tunayoifahamu, lakini pia kibiblia, Mungu anaichukulia nchi kama mke. Nchi inapomwasi Bwana (yaani mume wake) na kwenda kwa miungu mingine, basi inakuwa inafanya uzinzi). Pia Mungu anasema: Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa BWANA. (Kumb 18:10-12). Cha kusikitisha ni kuwa kuna hata makanisa yanayowaomba wafu. [Bibilia inasema: Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa. (Hosea 4:6)]. Ndugu, usifanye tu mambo kwa kuwa tu kiongozi mkubwa wa dini amesema ufanye. Tambua kuwa andiko hapo juu halisemi "wanaangamia" kama wengi ambavyo husema; linasema "wanaangamizwa". Hakikisha kwanza mambo hayo kwenye Biblia ndipo uyafanye. Neno “sikujua” halitakuwa kamwe moja ya utetezi katika siku ya mwisho. Mungu anatuasa kupitia nabii Isaya, akisema: Na wakati watakapokuambia, Tazama habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai? (Isaya 8:19). Alikuwapo mfalme wa Israeli ambaye aliitwa Manase. Mungu alikuwa na hasira naye kwa sababu ya mambo haya ya kuwaendea waganga. Imeandikwa: Tena akawapitisha wanawe motoni katika bonde la mwana wa Hinomu; akatazama bao, akabashiri, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa BWANA, hata kumkasirisha. (2 Mambo ya Nyakati 33:6). Unapoenda kwa mganga, anakuwa ananong’onanong’ona maneno usiyoweza hata kuyaelewa. Unadhani ni upuuzi tu? Hapana. Mwenzako anafanya mawasiliano kamili na mashetani walio katika ulimwengu wa roho. Uhusiano kati ya ulimwengu wa mwili (yaani wa wanadamu) na ulimwengu wa kiroho ni uhusiano wa kimikataba na kimaagano. Yaani ili uwasiliane au upate kitu kutoka kwenye ulimwengu wa kiroho, ni lazima utimize sheria fulani. Sasa, mikataba hiyo hufungwa kwa njia ya sadaka/dhabihu. Na mara nyingi sadaka hizo huwa ni za damu. Hatuwezi kuelewa kwa undani sana uzito wa damu katika ulimwengu wa roho, lakini ina nguvu sana. Kwa kifupi, damu ndiyo uhai. Maandiko yanasema: Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu. (Mambo ya Walawi 17:11). Unaweza kumpa mtu kila zawadi, lakini kama ukimpa uhai wako, nadhani hiyo itakuwa ni zawadi inayozidi zote. Imeandikwa: Msile kitu chochote pamoja na damu yake. (Law 19:26). Sasa kama unapenda kisusio, ni bora ujitafakari upya. Labda utasema, “Ah, haya si yalikuwa mambo ya agano la kale tu?” Baada ya Yesu kuondoka duniani, mitume wake waliwahi kukaa kikao mjini Yerusalemu kujadili mambo kadha wa kadha. Katika maamuzi waliyopitisha, wakasema tusiwabebeshe wale wasio Wayahudi sheria zitakazokuwa mzigo kwao, bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu. (Matendo ya Mitume 15:20). Kusongolewa ni kunyongwa, hivyo damu inagandia humohumo ndani ya mwili. Zamani kabla Yesu hajaja na kufa, Wayahudi walilazimika kutoa sadaka kwa kuchinja wanyama ili kumwaga damu kwa ajili ya kusamehewa dhambi zao. Na sheria ya Mungu inasema hivi: Kisha mtu awaye yote wa nyumba ya Israeli; au miongoni mwa wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yoyote nitakunja uso wangu juu ya mtu huyo alaye damu, nami nitamkatilia mbali na watu wake. (Mambo ya Walawi 17:10). Kwa nini anasema hivi? Ni kwa sababu: nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho juu ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi. (Mambo ya Walawi 17:11). Kwa hiyo, unapopeleka damu kwa mganga wa kienyeji, iwe ni kupitia kuchanjwa chale, kutoa kuku, au mbuzi, au sadaka ya juu kabisa (mwanadamu), unaingizwa kwenye mikataba au maagano na mashetani, hata kama akilini mwako wewe hukusema hivyo na hujui. Unakuwa wa kwao! Kunakuwa na kupatana kati ya nafsi yako na shetani. Simaanishi kuwa hutafanikiwa. La hasha! Utafanikiwa na utaona matokeo ambayo umeyatarajia. Lakini Biblia inasema hivi: Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje? (Mt 12:26). Waulize waganga wanaoweza kukuambia. Huwa hawatoi pepo. Anachofanya anakupa pepo kubwa zaidi ili kumtuliza yule mdogo. Lakini baada ya muda na hilo nalo linaanza kukuletea mateso; maana asili, wajibu na kazi yao ni uharibifu. Ulinzi si asili yao! Kwa sasa hutajua maana au madhara yake. Lakini kama hukutangua mikataba uliyoingia na ufalme wa giza, mara tu utakapovuka ng’ambo ya maisha haya, yaani ukifa tu, palepale kila kitu kinakuwa wazi kabisa. Unadhani ni kwa nini baadhi ya watu huhangaika sana wakati wa kufa, ilihali wengine wanakufa kwa utulivu tu? Wengi wao anakuwa ameshaona kule aendako, sasa anakuwa anajaribu kupambana ili asiende kule. Wale wa upande anakohusika wanakuwa tayari wameshafika pale kumchukua. Sasa kama ni wale wabaya, ndio mtu anaanza kujaribu kushindana. Kwenye ulimwengu wa roho kila kitu ni dhahiri kabisa. Mungu hutuonya juu ya kila kitu cha hatari lakini kamwe huwa hatulazimishi kutii. Utii ni uamuzi wako binafsi. Anachofanya baada ya kuonya ni kukungoja mwisho wa safari. Huko ndipo kuna kutoa hesabu. Kuhusiana na mtu aliyewatumainia waganga, pale mambo yatakapofika ukomo, BWANA anamwambia: Simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako; labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda. Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wajuao falaki, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata. Tazama, watakuwa kama mabua makavu; moto utawateketeza; hawatajiokoa na nguvu za mwali wa moto; hautakuwa kaa la kukota moto wa kukaa karibu nao. Ndivyo yatakavyokuwa mambo hayo uliyojitaabisha nayo; wale waliofanya biashara nawe tangu ujana wako watatanga-tanga mbali nawe, kila mtu akienda zake; hapatakuwa na mtu wa kukuokoa. (Isaya 47:12-15). Watu wajuao falaki, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, kwa kifupi ni hawa tunaowaita wasoma nyota. Hao ni machukizo mbele za Mungu, na hataki kamwe tuwaendee. Je, nawe ni mmoja wa watu wanaosoma nyota kwenye magazeti kila mwezi au kila siku ili kuangalia “bahati” yako imekaaje? Huo ni mtego wa kutoka kuzimu. Jiepushe nao. Sasa unafanyaje? Yesu anaitwa Mwana-Kondoo wa Mungu kwa sababu alitolewa kafara kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote. Na kwa sababu torati inasema uhai umo kwenye hiyo damu; damu ya Yesu ndio uhai wake, yaani alitoa uhai wake. Ukiingia ndani yake na kumwamini kama Mwokozi wako, unafunikwa na damu yake (uhai wake). Uhai huu ni moto mbele ya mashetani na wachawi. Kwa hiyo, unakuwa ni mmojawapo wa wale wanaofaidi ulinzi wa kiungu ambao una nguvu dhidi ya ibilisi na majeshi yake, na wakala wake wa kibinadamu. Imeandikwa: Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, wala hapana uganga juu ya Israeli. (Hesabu 23:23). Myahudi si tu yule wa Israeli, bali ni mtu yeyote ambaye Yesu ni Bwana na Mwokozi wake. Wanga wote waliowahi kucheza na watu wa aina hii, wanajua vizuri maana ya andiko hili. Ndugu, Mungu si wa mchezo. Ni ngao kwelikweli. Hapa tena anasema: BWANA, mkombozi wako, yeye akliyekuumba tumboni, asema hivi; Mimi ni BWANA, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke yangu; niienezaye nchi; ni nani aliye pamoja nami? Nizitanguaye ishara za waongo, na kuwatia waganga wazimu; niwarudishaye nyuma wenye hekima, na kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga; nilithibitishaye neno la mtumishi wangu, na kuyafikiliza mashauri ya wajumbe wangu. (Isaya 44:24-26). Karibu kwa Yesu. Acha kujifariji kwa dini. Je, unatambua kuwa Yesu hakuwa mkristo wala hakuleta ukristo? Yesu alikuja kuchukua dhambi za ulimwengu ili wanadamu wote wapone. Mambo ya dini yalianzishwa na wanadamu baadaye. Dini si mbaya, lakini si kitu cha msingi! Utakuwa na dini lakini bado wanga watakuwangia tu! Kuvaa hirizi na kuzindika kila kitu ni kumwekea shetani mteremko wa kushukia kwa ulaini maishani mwako! Usalama uko kwa Yesu si kwenye dini; na zaidi sana, si kwenye hirizi na uongo wa waganga wa kienyeji!

The revelation life

Maisha ya Maonyesho na Ubatili Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? (Yeremia 17:9). Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. (Wagalatia 6:4). Katika somo lililopita nililoliita Nia ya Ndani ya Moyo niligusia kuhusu umuhimu wa kuwa makini na nia zetu pale tunapomwendea Mungu, maana Mungu anajali sana hizo nia ambazo ndizo zinazoamua endapo atayakubali maombi yetu au tutaishia kupata hasara. Katika somo hili namwomba Mungu anisaidie kufafanua kwa uwazi zaidi kile ambacho hasa kinaweza kuwa kinaendelea ndani ya mioyo yetu, ambacho ndicho anachokiona Mungu wetu pale anapotutazama. Katika nyakati za Biblia kulikuwa na dhambi ambazo, labda niziite kuwa ni “za jumuiya.” Dhambi za namna hii zingeweza kutendwa na mtu mmoja lakini athari zake zikaangukia familia au hata taifa zima – ingawaje wengine wanakuwa hata hawakushiriki au hawakujua kwamba mkosaji halisi alikuwa anatenda dhambi hiyo. Kwa mfano, Mfalme Daudi alipofanya kosa la kuwahesabu Israeli, alisababisha vifo kwa watu ambao hawakuhusika na kosa lake. Imeandikwa: Basi Bwana akawaletea Israeli tauni tangu asubuhi hata wakati ulioamriwa; nao wakafa watu toka Dani mpaka Beer-sheba sabini elfu (2 Samweli 24:15). Pia, tunasoma kuhusu wana wa Israeli kwa ujumla kuhesabika kuwa wametenda dhambi kutokana na kosa la mtu mmoja, yaani Akani. Matokeo yake walishindwa kwenye vita na kakabila kadogo sana ka Ai. Imeandikwa: Lakini wana wa Israeli walifanya dhambi katika kitu kilichowekwa wakfu; maana Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila ya Yuda, alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; hasira ya Bwana ikawaka juu ya wana wa Israeli. (Joshua 7:1). Mbali na hivyo, kosa la Akani pia lilisababisha kuangamia kwa familia yake yote. Imeandikwa: Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na lile joho, na ile kabari ya dhahabu, na wanawe, na binti zake, na ng'ombe zake, na punda zake, na kondoo zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde la Akori. Yoshua akasema, Mbona umetufadhaisha hivi? Bwana atakufadhaisha wewe leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto, na kuwapiga kwa mawe. (Yoshua 7:24-25). Lakini ilifika mahali ambapo Bwana akasema: Tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapoipanda nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda, mbegu ya mwanadamu na mbegu ya mnyama. … Siku zile, hawatasema tena, Baba za watu wamekula zabibu kali, na meno ya watoto wao yametiwa ganzi. Bali kila mtu atakufa kwa sababu ya uovu wake mwenyewe; kila mtu alaye zabibu kali, meno yake yatatiwa ganzi. (Yeremia 31:27, 29-30). Na tena, ingawaje tunatakiwa kabisa kubebeana mizigo, kwa maana ya kusaidiana kwa upendo ili kuleta furaha, amani, uponyaji, n.k., lakini inapokuja kwenye hatima ya suala la dhambi na athari zake kwa yule azitendaye, imeandikwa: … kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe. (Wagalatia 6:5). Ndugu zangu, ninachotaka kusema hapa ni kwamba, Mungu anatupima kibinafsi katika kila jambo tunalojihusisha nalo hapa duniani. Kama ambavyo unaona kwamba ukinunua muda wa maongezi kwenye simu, hauwezi kamwe kuidanganya mitambo ili kwamba eti uongee hata kwa nusu sekunde na usikatwe pesa. Haiwezeani! Ukibonyeza tu, hata kama ingekuwa ni usiku wa manane, lazima mtambo utatambua na pesa yako itakatwa mara moja kulingana na kiwango cha upigaji simu wako! Hiyo ni teknolojia ya kibinadamu. Mungu ni zaidi! Hakuna sekunde yoyote katika maisha yetu inayompita. Hakuna!! Na kila kitu kinawekwa kumbukumbu mbinguni – kiwe ni tendo linaloonekana kwa nje au ni wazo lililojificha moyoni!! Ndiyo maana imeandikwa kwamba Mungu atazihukumu siri za wanadamu (Warumi 2:16). Je, ni kwa nini unafanya yale unayoyafanya? Hakuna mwanadamu anayejua kile kinachoendelea moyoni mwako. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? (1 Wakorintho 2:11). Roho yako, au wewe mwenyewe (pamoja na Bwana) ndio mnaojua kile kinachoendelea ndani ya moyo wako. Na kwangu vivyo hivyo! Na kwa mwingine vilevile! Sasa, kwa nini unafanya yale unayoyafanya? Nia yako ni nini? Katika mambo ya kawaida kabisa ya kila siku maishani mwetu ni lazima kujiuliza swali hili: Kwa nini ninafanya hivi? Makusudi yangu ni nini? Kwa nini unataka nguo ya gharama kubwa wakati ziko za gharama ndogo za ubora uleule? Kwa nini unataka uwe na magari kumi? Kwa nini unataka kumiliki maduka matano? Kwa nini unachubua ngozi yako? Kwa nini umebadili rangi ya nywele zako? Kwa nini umechora ‘tattoo’ kwenye mwili wako? Kwa nini unavaa mavazi yanayoacha wazi sehemu za mwili wako ambazo hazitakiwi kuachwa wazi? Kwa nini umevaa mlegezo? Kwa nini ulitoa mchango mkubwa sana kwenye harusi ya yule ndugu? Kwa nini umevaa nyusi za bandia? Kwa nini ukiwa kanisani unaonyesha sura ya unyenyekevu lakini ukiwa nje haufanyi hivyo? Simu yako ni ya gharama. Kwa nini unapenda kuitoatoa mbele za watu hata kama haupigi au haujapigiwa? Kwa nini umevaa cheni na unafungua vifungo vya shati lako? Kwa nini umevaa nguo inayoacha maziwa nje? Kwa nini ulimsaidia yule mtu aliyeomba msaada? Mengi ya mambo haya ni ya kawaida kabisa katika maisha yetu ya kila siku na hayana ubaya hata kidogo!! Hakuna ubaya kuwa na magari kumi, nyumba tano, simu ya shilingi milioni moja, n.k. Hakuna ubaya! Swali hapa ni moja tu: Moyo wako au moyo wangu unakuwa unanisukumaje mbele za watu? Kwa lugha rahisi, je, ninapenda kujionyesha? Ninaona fahari fulani watu ‘wanaponitambua’? Ninakuwa na shauku kila mtu ajue kuwa mimi ni wa kiwango cha juu? Je, kila wakati nakuwa naangalia kwa jicho la chati ili kubaini kama kuna watu wananitupia angalau jicho sawasawa na ninavyotamani wafanye? Ni hakika kabisa hivi ndivyo maisha ya wengi wetu yalivyo. Ni maisha ya maonyesho, maonyesho, maonyesho tu! Ni maisha ya kusaka sifa na umaarufu! Ni maisha bandia! Hatumfikirii Bwana bali tunawafikiria wanadamu. Tunatamani kusifiwa na wanadamu. Kwa watu wa dunia hii ni sawa kabisa. Lakini je, kwa Mungu nako ni sawa? Kwa wapendwa nako inatakiwa iwe hivyo? Je, kanisa litatofautishwaje na dunia kama nalo linafanya mambo haya? Je, ni kwa kiasi gani haujanaswa na mtego huu? Ni kwa kiasi gani haujaingia kwenye kapu hili? Kwa nini unafanya yale unayoyafanya? Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. (Wagalatia 6:4). Labda binti au msichana unasema, “Sasa nisipojipodoa na kujipamba nitapataje mume?” Dada yangu, kama Mungu ni Baba yako, basi lia na Yeye. Kibinadamu unaonekana kuna mantiki kabisa. Inaonekana kana kwamba usipojihangaisha kwa namna Fulani, basi utakosa mume. Lakini Bwana anapotutazama anasikitika kwa sababu hayo si maagizo yake. Maagizo yake yanasema: Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona. (2 Wakorintho 5:7). Kwa kuwa: Mwenye haki ataishi kwa imani. (Warumi 1:17). Jambo moja la msingi sana, si kwa akina dada tu, bali kwa kila mwanadamu, ni kufika mahali pa KUAMUA kuwa, “Mimi nitasimama na Bwana peke yake! Awe amenipa kile ninachokiomba au hakunipa. Basi!!” Huku ndiko kuyatoa maisha YOTE kwa Bwana. Lakini hii haitufanyi tuache kuomba kwa bidii zote yale ambayo mioyo yetu ina shauku nayo. Ni hasara sana kuishi maisha ambayo yanataka tu kuwavutia wanadamu na kutaka kusifiwa nao. Hayo ni maisha ya UBATILI mkubwa. Bwana anatuagiza katika sura ya sita ya Kitabu cha Mathayo: 1 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. 2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. 3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; 4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. 5 Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. 6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. 7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. 8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. (Mathayo 6:1-8). Japo hapa Bwana anaongelea zaidi suala la utoaji sadaka na maombi, lakini, kimsingi, yuko kinyume na maisha ya maonyesho mbele za watu. Tukifanya mambo kwa nia ya kuonekana mbele za watu ni kweli kabisa tutafanikiwa katika hilo. Tutasifiwa na kupata umaarufu huu batili wa dunia. Lakini hiyo ndiyo itakuwa thawabu yetu. Simaanishi kuwa sasa basi uwe mchafumchafu kwa sababu tu eti hauko hapa kuifurahisha dunia bali Bwana! La hasha! Uchafu pia ni dhambi. Ninachomaanisha ni mtu kufanya mambo yake hasa kwa ajili ya Bwana. Ni kufika mahali ambapo kila kitu ninachofanya ni kwa ajili ya kumtukuza Bwana wangu, Yesu Kristo. Kama kwa jambo hilo dunia itanisifu, sawa. Kama haitanisifu, nako sawa pia. Lakini kusifiwa na wanadamu kusiwe ndio sababu ya msingi inayonisukuma kufanya jambo lolote. Bwana anaagiza: Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu. (1 Wakorintho 10:31). Siamini kamwe kwamba mtu aliyeamua kwa dhati kuyafanya yote kwa utukufu wa Mungu atahangaika na mambo haya. Tunahangaika nayo kwa kuwa tu tumenaswa na ubatili wa dunia. Ni nani yuko tayari kumwangalia Bwana pekee na kuachana na ulimwengu huu? Ni nani ee Bwana aliye tayari kutafuta kwa bidii sifa kutoka kwako badala ya sifa za wanadamu? Ni nani aliye tayari ee Bwana kujikagua katika KILA wazo, neno na tendo, KILA sekunde ya maisha yake? Hakika yake Bwana hatuwezi. Hatuwezi kabisa bila neema yako. Tusaidie kuishi maisha matakatifu badala ya kushiriki na kuwa sehemu ya giza la dunia hii. Maana umesema kuwa sisi ni nuru ya ulimwengu. Lakini badala yake tumemezwa na giza; na sasa tunatafuta kila sababu [hata za kimaandiko] za kuhalalisha mambo haya ya giza. Tupe ufunuo wa rohoni ee Roho Mtakatifu ili tujue umuhimu na kuwa na utayari wa kubadilishwa na kupewa mioyo mipya inayoweza kukutii. Ni katika jina la Yesu naomba. Amina.

Ushuhuda wa Adelaida Juu ya Mbingu na Kuzimu


Mwanamke mmoja kutoka Bolivia aitwaye Adelaida De Carrillo alipelekwa Mbinguni na Kuzimu na Yesu Kristo. Kule alionyeshwa ni Utakatifu gani anaotakiwa mtu kuwa nao ili aweze kuingia kwenye UFALME WA MUNGU, na pia ni dhambi gani (ambazo wengi wetu tunadhani kuwa ni ndogo), zinaweza kumfanya mtu aingie Jehanamu.

Tuko kwenye safari ya maisha ya kimwili hapa duniani tukielekea kwenye maisha ya kiroho kwenye ulimwengu ule ujao. Huo ni ulimwengu halisi ambao una maisha halisi, utawala halisi na kanuni halisi za kuingia huko.
Wakati ulimwengu tuaoishi leo una serikali nyigi na watawala wengi, ulimwengu ule ujao utakuwa na serikali moja tu inayoongozwa na Yesu Krito. Wakazi wa uliwengu huo ni watakatifu WOTE!!!
Huo ni ulimwengu unaoongozwa na Mungu mwenyewe kwa upendo na amani. Kule hakuna magonjwa, vita, njaa, na dhambi zingine zote. Tiketi ya kuingia kule ni moja tu: nayo ni kumwamini Yesu Kristo kama Mwokozi aliyekufa na kufufuka kwa ajili yetu. Kisha tunaishi hapa duniani kwa kutii maagizo yake.  
Hata hivyo, wale wote ambao hawatakuwa wamestahili kuingia kwenye ulimwengu huo (kutokana na wao kuishi maisha ya dhambi na uasi dhidi ya sheria za Mungu hapa duniani), watatupwa nje ya mbingu kweny giza na moto, yaani kwenye jehanamu ya milele.
Katika ushuhuda huu, tunaona kile ambacho Bwana Yesu anatuagiza ili tuweze kustahili kuingia kwenye ufalme ule ujao na kuishi na Mungu MILELE!!!
Adelaida De Carrillo anasema:
HATUA YA 1: Ilianzia Kanisani kwenye wakati wa Huduma
Katika Ezekieli 36:25-26, Biblia inasema:
“Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote.  Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.”
Ushuhuda wangu uko namna hii: Siku moja ya Jumapili, kwenye saa 3 hivi, Kanisa letu lilikuwa na kipindi cha Huduma. Mungu alikuwa akimimina baraka zake juu yetu. Mchungaji wangu aliniambia,  “Adelaida, Bwana ananiambia nikupake mafuta.”
Aliweka mafuta mengi kwenye viganja vya mikono yake na akaanza kunipaka mwilini. Alinipaka masikioni, miguuni, tumboni na kwenye mwili wangu wote. Alipoweka mikono yake kwenye uso wangu, niliona mwanga mkubwa ukija kutokea juu, ukinielekea mimi. Kuanzia hapo nilipoteza fahamu na sikujua kilichokuwa kinaendelea kwangu.
HATUA YA 2: Safari Yangu Kwenda Mbinguni
Malaika walikuja na kunichukua tukaenda juu pamoja nao. Walianza kupambana na mashetani maana njia yetu ilikuwa imewekewa vizuizi. Kulikuwa na blangeti jeusi kwenye mawingu, likiwa limejaa mapepo yaliyojaribu kutuzuia kupita. Baadaye niliona mwanga mweupe kutoka Mbinguni na malaika mzuri sana akiwa na upanga wenye nuru mkononi mwake.  Aliinua upanga wake na kuanza kupigana na mapepo yale ili sisi tupite. Malaika yule alionekana kama Mwana wa Mfalme. Alikuwa na bamba la dhahabu kifuani mwake na nguo nzuri sana. Nywele zake zilikuwa za rangi ya dhahabu, na uso wake ulikuwa kama miali ya mwanga. Alikuwa mzuri sana! 
HATUA YA 3: Kuoshwa na Kubadilishwa Moyo Wangu
Malaika walikuja na kunichukua tukaenda juu pamoja nao. Walianza kupambana na mashetani maana njia yetu ilikuwa imewekewa vizuizi. Kulikuwa na blangeti jeusi kwenye mawingu, likiwa limejaa mapepo yaliyojaribu kutuzuia kupita. Baadaye niliona mwanga mweupe kutoka Mbinguni na malaika mzuri sana akiwa na upanga wenye nuru mkononi mwake.  Aliinua upanga wake na kuanza kupigana na mapepo yale ili sisi tupite. Malaika yule alionekana kama Mwana wa Mfalme. Alikuwa na bamba la dhahabu kifuani mwake na nguo nzuri sana. Nywele zake zilikuwa za rangi ya dhahabu, na uso wake ulikuwa kama miali ya mwanga. Alikuwa mzuri sana! 
Ghafla, nilisikia sauti ndani yangu, ikisema, “Nataka ufahamu kuwa nilikupa magoti hayo ili uwe mwanamke wa maombi, na si kwa ajili ya kuzungukazunguka ukifanya mambo yasiyonipendeza Mimi. Magoti haya ulipewa ili kufanya maombezi kwa ajili ya Kanisa. Ulitakiwa kulijua hilo.” 
Kwa ujumla mimi nilikuwa si mwanamke wa maombi sana. Maombi yangu yalikuwa na kawaida ya kuwa mafupi sana. Lakini Bwana alitaka niwe mwombaji zaidi. 
Malaika aliendelea kuosha miguu yangu, huku akiiparua, na mimi nilikuwa namlilia Mungu anihurumie kutokana na maumivu yale. Bwana akasema: “Miguu hii ulipewa ili uwe unazunguka kwenda kuhubiri Injili yangu, kueneza Neno langu na si kuzungukazunguka kwa majirani zako kupeleka umbeya, na kufanya mambo ambayo hayanipendezi Mimi. Na kwa sababu hii,” Bwana akasema, “ninasafisha miguu yako.”
Jambo hili liliendelea na lilifanyika kwa maumivu makali sana. Bwana akasema, “Hii ni muhimu sana ili uweze kuelewa mipango niliyo nayo kwa ajili yako.”
Baadaye, nilipelekwa kwenye sehemu nyingine ambako malaika wngine watatu walikuwa wananingojea. Sehemu hii ilikuwa tofauti. Niliona vitu kama mashine. Malaika wale walianza mchakato mwingine wa kusafisha macho yangu kwa kutumia aina fulani ya mafuta. Nilihisi kama vile macho yameng’olewa kutoka kwenye matundu yake. Nikasema: “Tafadhali mnihurumie. Naomba msaada. Kwa nini mnanifanyia hivi?” Ilikuwa kama vile wanakwangua macho yangu. Kitu kama samaki kilitolewa kutoka kwenye macho yangu.
Bwana akasema, “Binti yangu, nafanya hivi kwa ajili yako kwa sababu nataka ubadilike. Mambo uliyokuwa ukifanya duniani hayakuwa yakinipendeza. Sikuwa nafurahi ukiwa duniani ulipokuwa ukitazama mambo ambayo hayakunipendeza Mimi. Ulikuwa ukitazama TV”  [Soap Operas]  ... “Hayo hayajengi maisha yako.”   ...  “Sifurahii pale wanangu wanapoangalia vitu kama hivyo; vitu ambavyo havinipi utukufu.”
Nikasema, “Bwana, nisamehe. Naomba rehema zako.” Na Bwana akasema, “Katikati ya usiku kwenye saa sita, mara zote huwa uko macho ukiangalia sinema ambazo hazikujengi wewe; na nyingi ya sinema hizo zimejazwa mambo mengi yanayohusu mapenzi. Sikukupa macho hayo kwa ajili ya mambo kama hayo. Nilikupa hayo macho ili utazame mambo yale tu yanayonipa Mimi utukufu. Na kwa sababu hii ndiyo maana ninasafisha macho yako.” 
Malaika waliendelea kusafisha macho yangu huku mimi nikiendelea kuomba kuhurumiwa. Baadaye macho yangu yalipakwa mafuta, na kuanzia hapo nikawa na mtazamo tofauti; macho yangu yalibadilishwa kabisa. Bwana akasema, “Usitamani waume wa watu wengine tena!”  Mimi nilikuwa na kawaida ya kuvutiwa sana na wanaume wengine, na Bwana alisema kuwa mambo hayo hayampendezi.
Nitakueleza mimi nilikuwa mtu wa namna gani. Nilikuwa Mkristo duni wa kilokole ambaye alikuwa hatendi mambo sawasawa na Biblia inavyoagiza. Kila nilichofanya kilikuwa ni kutokana na matamanio yangu na njia zangu binafsi, kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu. Nakueleza haya ili uweze kurekebisha njia zako; ili roho ziweze kuokolewa. Nakueleza kuwa tamaa NI dhambi; kuangalia michezo ya kwenye TV [Soap Operas], sinema za kidunia – mambo yote haya hayampendezi Mungu.
Malaika waliendelea na mchakato wa usafishaji. Walikuwa na kijifimbo kidogo cha kioo ambacho walikiingiza moja kwa moja masikioni mwangu. Walipoanza kukwangua masikio yangu, nilihisi maumivu makali sana. Moyo wangu ulihisi maumivu haya yote. Mara maji meusi yalianza kutoka kwenye masikio yangu, na baadaye maji ya rangi ya kijivu. Niliendelea kulia. 
Bwana akasema, “Binti yangu, ninasafisha masikio yako kwa sababu ulipenda sana kusikiliza mambo ambayo hayanipendezi Mimi. Ulipenda kusikiliza umbeya. Uliyatoa kabisa masikio yako kusikiliza mambo yasiyonipendeza Mimi. Baadhi ya watu wanakuja kwako kuleta umbeya na wewe ulipenda kuwasikiliza hata kama walileta umbeya dhidi ya Mchungaji wako mwenyewe. Ulipenda kuwasikiliza hao. Badala ya kumtetea Mchungaji wako na kumsahihisha mbeya huyo ili arekebishe njia zake, ulikuwa kama wao, ukifanya umbeya pamoja nao. Usisikilize umbeya tena. Mtu akija kwako na umbeya wa aina yoyote, waombe radhi, kisha ondoka mara moja bila kushiriki. Usisikilize tena mambo yasiyokujenga!”
Nikasema: “Bwana, nisamehe!” Nilijua kuwa nilikuwa nina hatia. Hakuna jambo lililofichika mbele za Mungu. Hakuna anayeweza kujificha mbele zake. Kila tunachofanya na kusema hapa duniani kimewekwa kumbukumbu Mbinguni. Kutokana na maumivu yote yale masikioni mwangu, nikasema: “Bwana, nisamehe. Naomba rehema zako.”  Hatimaye masikio yangu yalipakwa mafuta na malaika.
Bwana akaniambia: “Kuanzia leo na kuendelea, utasikiliza tu mambo ambayo nimekuruhusu kusikiliza. Utafanya mambo yale tu ambayo nimekutaka ufanye; hautakuwa Adelaida wa zamani tena. Hivi sasa wewe ni mtu mpya na ni lazima uwe ni mwanamke yule ambaye ninataka uwe.”
Baada ya hapo nilipelekwa kwenye idara nyingine ambako malaika walianza kusafisha kinywa changu. Ulimi wangu ulitolewa kabisa kinywani na kuwekwa kwenye aina fulani ya sinia. Malaika alianza kusafisha ulimi wangu, na hapa tena nilihisi maumivu makali sana. Bwana akasema: “Nataka kukusafisha. Nataka kukusafisha.”
Malaika walivyokuwa wanakwangua ulimi wangu, maji meusi yalikuwa yanatoka humo, na baadaye yalitoka maji meupe. Mwishowe malaika walitumia maji matamu sana kuoshea ulimi wangu. Yalikuwa matamu mno. Hakuna kitu duniani kinachoweza kulinganishwa na utamu wa maji yale. Kisha ulimi wangu ulipakwa mafuta. Kinywa changu nacho kilipitia mchakato huohuo. Maji meusi yalitoka kwenye kinywa changu.
Bwana akasema, “Binti yangu, ninafanya hivi kwa ajili yako ili usifanye umbeya tena; ili uache kufanya mambo yasiyonipendeza; maana ulimi wako ulishiriki katika mambo mengi sana ambayo hayanipi utukufu Mimi. Ulisema uongo mwingi sana. Acha kusema uongo! Kusema uongo hakutoki kwangu. Waongo hawanipendezi Mimi. Waongo wote hawataniona Mimi. Hakuna mwongo atakayeingia kwenye Ufalme wa Mbinguni.”
Nikasema: “Bwana, nihurumie. Najua kuwa nilifanya mambo hayo yote. Nilisema uongo mara nyingi, lakini tafadhali nisamehe.” Nilisema yote haya kwa sababu ya maumivu niliyokuwa nayahisi.
Bwana akasema: “Ninafanya hivi kwa sababu ninakupenda. Ukiendelea na hali uliyokuwa nayo, nitakupoteza. Kama nisingefanya yote haya, usingebadilika kamwe. Ni lazima niokoe moyo wako na hii ndiyo sababu ya kufanya yote haya. Nakupenda, na kwa sababu nakupenda, sitaki kukupoteza.”
Bwana akasema tena: “Kama ulivyo wewe, wengi kati ya watu wangu wako namna hiyohiyo.Wanasema uongo, wanaishi maisha ya aina mbilimbili, na wanaonekana wako safi mbele ya watu wengine. Unapomwinulia mumeo sauti ulimi wako unakuwa unatumiwa pia.” Kinywa changu kilitakaswa kabisa. Halafu Bwana akaniambia nimeze maji hayo. Nami nikafanya hivyo.
Ulimi wangu na kinywa changu vilipakwa mafuta ya thamani sana ya mbinguni. Mafuta hayo yalikuwa maalum sana, yakiwa na harufu ya thamani sana. Hayawezi kulinganishwa na mafuta yoyote ya hapa duniani. Ulimi wangu ulirudishwa tena kinywani mwangu. Malaika mmoja alikuja na kuweka hatamu kwenye koo langu. Na Bwana akaniambia: “Hii ni sawa na vile farasi anavyowekewa hatamu.”
Nikwambie tu kwamba, hii ndiyo njia pekee tunayoweza kubadilishwa. Acha kuongea maneno machafu na kushiriki katika mambo ambayo hayatujengi. Mambo haya hayampendezi Mungu kamwe.
Acha kutamka maneno machafu na yasiyo na maana. Wako Wakristo wengi – akina kaka, dada, Wainjilisti, Wamisionari, n.k., ambao wanapenda kusema maneno machafu na yasiyo na maana. Niko hapa kukuhakikishia juu ya kile ambacho Bwana alinionyesha ili maisha yako yabadilishwe. Ushuhuda huu ni kwa ajili ya wewe kubadilika. Upendo wa Mungu na wa kwangu kwako ndio ulioleta ushuhuda huu.
Ulimi wangu ulirudishiwa tena mahali pake na malaika na ukawa umebadilishwa kabisa. Naweza kukuambia sasa, hakuna mtu anayeweza kunikasirisha tena. Sasa naweza kufanya yale tu yanayompendeza Mungu.
Kisha, pua yangu nayo ilipitia mchakato huohuo. Maji meusi yalitoka puani mwangu wakati wa kusafishwa na baadaye maji meupe. Pua yangu ilipakwa mafuta na nilihisi maumivu makali sana wakati wa mchakato wa kusafishwa. Nilisema: “Bwana, tafadhali niambie mambo niliyofanya kwa kutumia pua yangu ambayo hayakukupendeza.”
Bwana akaniambia: “Baadhi ya wateja wako huvuta sigara na wewe unavuta  ule moshi kupitia pua zako maana uliwahi kuwa mvutaji sigara na sasa wewe unajisikia vizuri kukaa nao wakati wanapovuta.” Nikasema: “Bwana, najua. Nisamehe. Naomba unirehemu.”
Bwana akaniambia: “Uko sawa tu na wale wote wanaovuta sigara na wote wanaokunywa pombe pale unapokaa nao na kuvuta harufu ya sigara na pombe.”
Bwana akasema tena: “Hii ndiyo sababu yangu ya kukusafisha wewe. Kwa hiyo, kuanzia leo kila utakapomwona mtu anavuta sigara au anakunywa pombe, hautajisikia vizuri kukaa nao tena. Utajisikia kinyaa.”
Hakuna cha kujitetea mbele za Bwana. Mungu anafahamu fika wewe ni nani na mimi ni nani. Libarikiwe Jina Takatifu la Bwana, Amina.
Niliendelea kumwomba Bwana rehema na nilipelekwa sehemu nyingine. Pale, malaika walianza kuosha mwili wangu uliobakia kwa kutumia sabuni nyeupe. Maji ya kijivu yalitoka kwenye mwili wangu.
Nikasema: “Bwana, nisaidie. Tafadhali, nisaidie.” Malaika walikuwa wanasugua mwili wangu na ngozi ya juu iliondoka. Damu ilikuwa inachuruzika kutoka kwenye ngozi yangu na nikamwuliza Bwana: “Kwa nini unanifanyia hivi?”
Bwana akaniambia: “Ninakusafisha. Ni lazima uwe safi mwili wako wote, nafsi yako, na roho yako. Roho yako, nafsi na mwili ni lazima viwe safi, asema Bwana.”
Sabuni ilisuuzwa kutoka kwenye ngozi yangu kwa kutumia maji ya thamani sana. Kisha malaika walipaka mafuta kila sehemu ya mwili wangu; kila sehemu ya mwili wangu. Sehemu zote za mwili wangu zilipakwa mafuta.
Bwana akaniambia: “Usirudi tena kwenye njia zako za zamani, binti yangu. Hivi sasa wewe ni Mtakatifu wangu aliyepakwa mafuta.”
Nikasema: “Bwana, nisamehe kwa mambo yote niliyokuwa nikifanya zamani hata mbele za uwepo wako. Nisamehe Bwana kwa kuwa kila kitu ambacho Mchungaji wangu alijaribu kunisahihisha mimi nilikuwa nikipingana naye. Nilisema mambo mengi kwake ambayo sikutakiwa kusema.”
Mchungaji wangu mara nyingi alikuwa akiniambia kuwa mavazi yangu kama Mkristo hayakuwa sawa. Nilishindana naye sana. Aliwahi kuniambia kuwa nilisema uongo na mimi nikahuzunika. Pale mtu anapopotoka na Mchungaji wake akamsahihisha, mtu huyo huhuzunika. Siku zote mimi nilikuwa kinyume na Mchungaji wangu.
Kisha nilipelekwa kwenye idara nyingine ambako nilipokelewa na malaika watatu. Malaika wale walitumia nguo nyeupe kufuta maji kwenye mwili wangu. Kwenye nyuso za malaika wale, niliona kuwa walikuwa wanajisikia huruma sana kwa ajili yangu kutokana na yote niliyopitia lakini hawakusema kitu chochote, hata neno moja. Sikuweza kumwona Bwana kwenye sehemu hizi. Nilikuwa nasikia tu sauti yake.
Malaika wengine watatu walinipokea kwenye idara nyingine. Malaika hawa walinivika nguo nyeupe ya juu na sketi ndefu. Sketi ilikuwa ndefu sana kiasi kwamba miguu yangu ilikuwa haionekani.
HATUA YA 4: Niliwaona Watakatifu Wengine Mbinguni
Nilipelekwa kwenye sehemu nyingine na mlango ulifunguliwa. Niliona mwanga mkubwa ukimulika kupitia mlango ule. Ulikuwa ni mwanga wa kuvutia sana. Bwana aliniambia nipite ndani. Nikasema, “Bwana, naogopa.”
Nilijua kuwa Mungu alikuwa ananiandaa kwa sababu anataka niokoke. Upendo haupendi mtu yeyote apotee. Nilisema: “Bwana, unirehemu.” Moyo wangu ulikumbuka vizuri sana kila kitu nilichoacha nyuma kule duniani; wanangu. Nikasema: “Bwana, naikabidhi familia yangu mikononi mwako.”
Kwenye sehemu ile niliweza kuona vitu kama miji mikubwa na watu wengi sana ambao walikuwa wananingojea. Walikuwa wananipungia mikono. Walikuwa wanataka niende kwenye sehemu ile walikokuwa.
Bwana akaniambia: “Mtakatifu wangu, muda umeshafika. Muda umefika wa kuwaona wote walio hapa ambao wanakungojea.” Watu wengi sana walikuwa wananingojea. Nami nilimwuliza Bwana: “Kitu gani kinaendelea hapa?”
Bwana akaniambia: “Ni wakati wa wewe kwenda na kuwahubiria watu wote. Ni wakati wa wewe kwenda na kuhubiria mataifa yote. Ni wakati umefika. Yote ambayo nimekuambia, nenda kawaambie Kanisa langu maana nitalifanya Kanisa langu kuwa kamilifu. Nitaifanya nyumba yangu kuwa kamilifu. Kisha Neno langu litapelekwa sehemu zote duniani zilizobakia, asema Bwana. Lakini kwanza ni Kanisa langu.”
Hatua Ya 5: Safari Yangu Kuzimu na Yote Niliyoyaona Kule
Malaika walinitoa pale na tukawa tunaelekea chini. Nikawauliza malaika wale: “Mnanipeleka wapi?” Niliingiwa na hofu kubwa sana na ghafla ardhi ilifunguka.
Nikauliza tena: “Mnanipeleka wapi? Kitu gani kinachoendelea kwangu?” Tuliingia moja kwa moja kwenye ardhi. Ilikuwa inatisha sana. Kila upande kulikuwa na giza, nami sikuelewa malaika wale walikuwa wananipeleka wapi.
Tulifika mahali ambako niliweza kuona mwanga mkali. Kulikuwa na mlango chini ya ardhi. Mlango ule ulikuwa mbaya sana. Hakuna kitu kwenye dunia hii kinachoweza kufananishwa na mlango ule.
Bwana akaniambia: “Huu ni mlango wa kuzimu.”
Nilifikiri labda ndio nilikuwa nimehukumiwa kutupwa kuzimu kwa yale yote niliyotenda zamani. Kulikuwa na mtu akiningoja pale. Bwana wetu Yesu Kristo ni mzuri sana. Bwana wetu Yesu Kristo alinyosha mkono wake kwangu. Alikuwa akiningoja kwenye mlango wa kuzimu huku akiwa na ufunguo. Na niliweza kuona wanyama wengi wa kutisha wakitokea kuzimu.
Nikasema: “Bwana, ni kitu gani kinachotokea kwangu? Tafadhali Bwana, nihurumie.”
Bwana akaniambia: “Nitakuonyesha kuzimu na kila kitu kilichomo ndani yake, ili uweze kuogopa na pia, kupitia wewe, watu wengine waweze kujua kuwa kuzimu kweli kupo.”
Nikasema: “Bwana, hapana. Sitaki kwenda humo!”
Bwana akasema: “Binti yangu, fuatana nami. Njoo.”
Tulipofika pale, baadhi ya mapepo yalinyosha mikono yao kujaribu kunikamata. Nikasema,  “Bwana, siwezi kuona, tafadhali.”  Nilijaribu kufunika uso wangu kwa mikono yangu, lakini bado nilikuwa naona kila kitu waziwazi. Ukiwa pale, unasikia kila kitu, unaona kila kitu na unagusa kila kitu, kama ilivyo kwa roho zingine zilizoko humo kuzimu. Bwana aliwazuia mapepo kunikamata. Nilikuwa niko na Bwana. Niliweza kuona jinsi roho zilizoko kuzimu zinavyoteseka.
KUNDI LA KWANZA LA ROHO NILILOONA KUZIMU: MASHOGA NA WASAGAJI
Bwana alinipeleka mahali fulani. Watu waliokuwa pale walikuwa ni Wakristo. Walimtumikia Bwana walipokuwa duniani lakini wakati huohuo walikuwa wakitenda mambo yasiyompendeza Mungu. Walikufa na sasa wako kuzimu.
Bwana alinionyesha mchungaji ambaye alikuwa akitumia vibaya Neno la Mungu. Mchungaji huyu alikuwa anafanya mapenzi na wanaume wenzake. Hakuwa mwana wa Mungu kwa sababu wana wa Mungu hawatendi mambo kama hayo. Hapohapo, niliweza kuona jinsi mapepo yalivyokuwa yanamtesa mchungaji yule ambaye alilinajisi Neno la Mungu. Mapepo yalimwingiza kwenye tyubu fulani, na tyubu hiyo ikaanza kumzungusha na kumzungusha! Alikuwa anateseka kweli! Alipokuwa duniani, alikuwa akinajisi watoto wadogo. Alinajisi hata wanaume wenzake.
Kama ambavyo unasoma ushuhuda huu, huenda haya ndiyo unayofanya. Kuzimu ni halisi na pia kuna adhabu inayowangoja wote wasiotii Neno la Mungu.
Mungu alikuumba wewe mwanamume. Pia, alimuumba mwanamke. Niliona jinsi mwanamume huyo alivyokuwa anateswa kuzimu. Roho yake ililipuka kisha ikajikusanya tena na kuendelea na mateso yale.
Bwana alimwambia: “Mwanangu, ulikuwa na muda wa kutosha duniani wa kutubu na kurekebisha njia zako.”
Bwana alimwonyesha skrini na kwenye skrini hiyo yalionekana maisha yake alipokuwa duniani. Alionekana mzee ambaye alikuwa akimwambia asifuate njia mbaya; akimwambia atii Neno la Mungu. Kila neno ambalo Bwana alimwambia kwa njia mbalimbali alionyeshwa kwenye skrini ile. Alikataa kutubu na kurekebisha njia zake.
Na siku moja, alipata ajali na akafa. Hivi sasa yuko kuzimu. Alijifanya kuwa yeye ni mchungaji kumbe hakuwa mchungaji. 
Bwana alimgeuzia mgongo na yule mtu akaanza kutukana. Hakuna upendo kuzimu. Hakuna kitu kabisa zaidi ya uchungu, huzuni, na maumivu ya kutisha ambayo hakuna mtu anayeweza kustahimili.
Wakati niko pale, nilijihisi kama nataka kufa. Nilisema: “Bwana, nataka kufa.”
Bwana akaniambia: “Binti yangu umeshakufa. Ona kile ambacho roho zinateseka kuzimu binti yangu.”
Nikasema: “Bwana, siwezi kuvumilia zaidi. Roho yangu inaungua. Joto ni kali sana. Bwana, siwezi!”
KUNDI LA PILI LA ROHO NILILOONA KUZIMU: MAKAHABA
Bwana alinipeleka sehemu nyingine. Niliona jinsi mapepo yanavyoitesa roho ya mwanamke mmoja kuzimu. Mwanamke huyu alikuwa ni kahaba wakati akiwa duniani. Aliwahi kuokoka. Bwana alimtoa kwenye ukahaba. Lakini alianguka tena na kurudia ukahaba ule na akawa katika hali mbaya kuliko mwanzo. Alikufa kwa kuuawa na sasa yuko kuzimu.
Niliona jinsi mapepo yalivyokuwa yanamtesa kuzimu. Badala ya kuolewa na kufanya mapenzi na mume mmoja tu, aliamua kufanya kinyume. Mungu anachukia mambo hayo yote. Hayo ni machukizo mbele za Mungu. Mwanamke yule alikuwa uchi. Alilazwa chini na mapepo walikuwa wanamteza. Nikasema: “Bwana, mhurumie.”
Bwana akasema: “Hapanaaa binti yangu. Alikuwa na muda wa kutosha duniani wa kutubu.” Bwana alimwonyesha skrini na wakaonekana Wainjilisti mbalimbali walioenda kumweleza juu ya kuyatoa maisha yake kwa Yesu. Lakini hakutii sauti ya Mungu. Hivi sasa yuko kuzimu. 
Ujumbe huu ni kwa wanawake wote wanaojiuza miili yao. Labda unafanya hivyo kwa ajili ya kupata fedha za kulisha wanao; labda huna mume. Mungu anakuambia leo urudi kwake. Mungu atakuhudumia wewe na familia yako. Kwa wanawake wote wanaouza miili yao, nawaambia kwamba, tubuni leo na kumrudia Mungu kupitia ushuhuda huu. Mungu ameleta ushuhuda huu kwa ajili ya wokovu wa roho zenu ili kwamba msije kuishia kwenye sehemu ile ya mateso.
KUNDI LA TATU LA ROHO NILILOONA KUZIMU: WAONGO NA WASENGENYAJI
Bwana alinipeleka kwenye sehemu nyingine waliko waongo na wasengenyaji. Niliona jinsi walivyokuwa wanateseka kuzimu. Ni hali ngumu mno. Ni vigumu mno kuongelea kuhusu kuzimu.
Usengenyaji unaweza kukufanya upoteze wokovu wako. Kuwasengenya majirani zako kunaweza kukupotezea wokovu. Kumsengenya mchungaji wako kuwaweza kukupotezea wokovu wako. Tubu leo kupitia ushuhuda huu na umrudie Mungu, na Mungu naye atakurudia wewe, asema Bwana.
Niliuliza: “Bwana, yaani hii ni kwa sababu ya usengenyaji tu?”
Bwana akasema: “Ndiyo, ni kwa usengenyaji tu.”
Nikauliza: “Bwana, lakini si huwa tunaomba rehema tunapokutenda dhambi?”
Bwana akasema: “Hapana. Watu hawa hawakuomba rehema; na sasa wanalipia dhambi zao.”
Kwa sababu hiyo, tunatakiwa kupatanishwa na Mungu kila siku kwa sababu hakuna ajuaye ni lini atakufa. Usiondoke uweponi mwa Mungu. Usengenyaji unaweza kukufanya upoteze wokovu wako.
KUNDI LA NNE LA ROHO NILILOONA KUZIMU: WAABUDU SANAMU
Mateso mahali pale yalikuwa makali sana. Kwa wanawake wote wanaomtumikia Maria Lionza, je, mnamjua ni nani huyo? Huyo ni pepo. Bwana alinionyesha  Maria Lionza ni nani. Ni pepo ambaye wachawi wengi wanapiga magoti kumwabudu kule kuzimu. Mapepo yaliwatesa kupita kiasi. [Maelezo ya blogger: Maria Lionza ni mzimu unaoabudiwa hasa kule Venezuela. Unaweza kusoma zaidi kwa kubofya HAPA.]
Miali ya moto wa kuzimu huwa haizimiki. Inawaka usiku na mchana. Inawaka milele. Tafadhali ningependa utambue hili: waabudu sanamu hawawezi kuuona uso wa Bwana.
Mungu anataka kubadili maisha yako. Mungu anataka uache kuabudu sanamu. Mungu anataka umwabudu Yeye tu. Kuna Mungu mmoja tu na zaidi yake hapana mwingine.
Roho za watu walio pale wanalazimishwa kumwabudu pepo huyo hata kama hawataki. Wanateswa sana. Wanalazimishwa kuvuta sigara kuzimu pale wanapomwabudu huyo pepo.
Shetani ni mwongo. Amekuja kuua na kuharibu. Lakini ni lazima nikuambie hili: Yesu Kristo alikuja kuleta uzima na uzima tele. Mungu Mwenyezi anakuita leo kupitia ushuhuda huu. Natamani uweze kuelewa ujumbe huu na mipango aliyo nayo Mungu kwa ajili yako. Mungu ni halisi.
Nilikuwa kuzimu kwa saa 16 ili kuelewa makusudi ya ujumbe huu; ili niweze kuuhubiri; ili niweze kusambaza ujumbe wa wokovu kwa kila mmoja kwa moyo wote.
Nilimwona Barbara. Nilimwona Shango. Ninyi mnaomwabudu Barbara, mtupeni nje ya nyumba zenu. Bwana anasema huyo ni pepola ukahaba.
Barbara hana upendo. Amejaa uharibifu. Ziko nyumba nyingi ambazo hazina amani. Yeye ndiye anayehusika na hilo. Pia, unaweza kuwa unashangaa ni nini kinachoendelea kwenye maisha yako – labda una sanamu yake kwenye nyumba yako. Natamani sana ungeelewa ujumbe huu na mpango wa Mungu kwa ajili yako. Pepo huyu alikuwa anawalazimisha watu kuzimu wamwabudu yeye. Watu pale wanateseka sana. Ni moto tu kila mahali. 
Nilimwuliza Bwana: “Je, hukuwapa watu hawa nafasi ya kurekebisha njia zao?”
Bwana akasema: “Niliwapa. Nilituma watakatifu wangu kwao.”
Palepale kuzimu skrini inawekwa mbele yao nao wanaonyeshwa kila kitu. Roho zilizo kuzimu hazina cha kujitetea mbele za Bwana. Bwana anawaonyesha kila fursa waliyopewa walipokuwa duniani. 
Kama hutatubu na kurekebisha njia zako leo, utaona jinsi kifo kitakavyokushangaza nawe utaishia kuzimu. 
KUNDI LA NNE LA ROHO NILILOONA KUZIMU: WALEVI
Bwana alinipeleka kwenye sehemu nyingine. Ilikuwa ni kama klabu kubwa. Nilisikia watu humo wakipiga kelele, huku wakiomba kuhurumiwa na kusaidiwa. Nikauliza: “Ni nini kinachoendelea humu?”
Bwana akasema: Peleka ujumbe huu kwa wote wanaotumia vileo usiku na mchana; kwa wote wale wanaoingiza miilini mwao vitu ambavyo haviwajengi; kwa wote ambao wanatumia hata fedha za watoto wao kwa ajili ya kulewea; peleka ujumbe huu kwa wanawake wale wote wanaolewa – waambie warekebishe njia zao kupitia ujumbe huu.”
Pale kuzimu niliona meza imewekwa mbele yao ili wanywe. Walilazimishwa kunywa bila kupenda. Wote walikuwa katikati ya moto. Kile walichokuwa wakinywa ni asidi nami niliona jinsi roho zao zinavyolipuka baada ya kunywa.
Nikasema: “Bwana, hapana. Siwezi kuvumilia zaidi ya hapa, tafadhali Bwana.”
Kuna mwanamume kuzimu ambaye, wakati angali duniani, Bwana alimpelekea Mwinjilisti baa akiwa analewa. Mwinjilisti yule alimwambia atoe maisha yake kwa Bwana wetu Yesu Kristo, maana Mwinjilisti yule alihisi kuwa mtu yule asingechukua muda mrefu kabla ya kufa. Mtu yule alimtukana Mwinjilisti huyo. Alimwita kuwa ni mwanamke mwenye wazimu, jambo ambalo watu wengi duniani wanawaambia Wakristo duniani. Siku ileile, mtu yule alitoka baa akiwa amelewa. Alipata ajali na sasa yuko kuzimu.
Alikuwa analazimishwa kunywa vinywaji vya kule kuzimu. Alijaribu kukimbia mateso lakini mapepo hayakumwachia. Anateswa pale kuzimu milele.
WAVUTA SIGARA
Wavuta sigara nao wana idara yao kule kuzimu. Wale wote wanaovuta bangi na wao pia wana idara yao kuzimu. Wanateswa milele.
KUABUDU AU KUHESHIMU SANAMU
Huenda unajiita Mkristo au vinginevyo, lakini bado unaheshimu au kuabudu sanamu. Ni lazima utubu leo na kuyatoa maisha yako kwa Yesu Kristo.
Kule kuzimu kuna wanaume na wanawake. Unaweza ukawa tajiri sana hapa duniani kama ukitaka. Utaenda kuzimu usipotaka kuyatoa maisha yako kwa Yesu Kristo. Fedha zako haziwezi kukununulia wokovu. Wokovu wako ulishanunuliwa na Bwana wetu, Yesu Kristo. Amina.
Alikuwapo mwanamume mwingine ambaye naye alikuwa analazimishwa kunywa kinywaji cha kuzimu. Nikamwuliza Bwana kwamba yule alikuwa nani.
Bwana akasema: “Mtu huyu alikuwa ni Mtakatifu wangu. Aliniacha na kuziendea njia zake na hatimaye alikufa katika dhambi.”
Kila kitu ambacho Bwana alikisema kuhusiana na mtu yule kilikuwa kinaonyeshwa kwenye skrini – ujumbe, siku na saa ambayo Bwana alimpelekea ujumbe. Mtu huyo yuko kuzimu sasa kutokana na uasi wake.
Unaweza kuwa unasema kwamba hii si kweli. Lakini niko hapa kukueleza kwamba Bwana wetu Yesu Kristo ni halisi.
KUNDI LA SITA LA ROHO NILILOONA KUZIMU: WANAWAKE WA MUNGU [WAHUBIRI]
Hawa ni wanawake waliomtumikia Mungu wakati wakiwa duniani. Lakini hawakutaka kubadilika na kukubaliana na mafundisho ya Mungu. Badala yake wao walipendelea kumtumikia Mungu kwa namna zao wenyewe. Mateso niliyoyaona hapa yalikuwa mabaya zaidi ya yale niliyoyaona kabla.
Nilisikia huzuni kubwa sana kwa ajili ya hawa wanawake wa Mungu walio kuzimu, maana walimtumikia Mungu wangali duniani.
Bwana aliniambia: “Kila wakati niliongea nao. Nilijaribu kuwarekebisha kupitia baadhi ya Watakatifu wangu lakini hawakutaka kuelewa makusudi.”
Bwana alinionyesha mmojawapo wa wanawake hawa. Alikuwa amekaa kwenye kiti na kiti kile kilikuwa kimezungukwa na moto. Ghafla pepo lilitokea na kummiminia maji fulani kichwani.
Bwana wetu Yesu Kristo alikuwa analia; Bwana wetu alikuwa analia.
Nikauliza: “Bwana, kwa nini unalia?”
Bwana akaniambia: “Niliteseka sana kwa ajili ya roho zilizoko kuzimu. Alikuwa ni Mtakatifu wangu. Nilimrekebisha ili asiipende dunia wala mambo ya dunia.” Bwana alikuwa anamsahihisha aache kupaka nywele zake rangi.
Bwana aliniambia: “Alikuwa anaonea aibu mvi nilizompa. Alikuwa anajaribu kujionyesha kwa mwonekano ambao si wa kwake.”
Nywele zangu zilikuwa nyeusi na mimi nilitaka ziwe nyeusi. Bwana akaniambia: “Usionee aibu kile ambacho nimekupatia.” Pepo liliendelea kumtesa. Alimlilia Bwana amsaidie. Bwana alimwambia kwamba alishachelewa. Akaanza kutukana.
Hatuwezi kuishi kwa kujificha uhalisia wetu. Siku moja sote tutakuwa na mvi.
Kadiri mapepo yalivyoendelea kummimina yale maji kichwani mwake, shingo yake ilipinda upande mmoja. Nywele zake zilikuwa zinadondoka. Alinyosha mikono yake ili kujaribu kuomba msaada. 
Nikasema: “Siwezi kuvumilia zaidi.”
Nilijaribu kufunika uso wangu maana hata mimi nilikuwa ninabadili rangi ya nywele zangu lakini sikuweza kuufunika uso wangu.
Bwana akaniambia: “Usionee aibu kile ambacho nimekupa.”
Mwanamke yule alikuwa na nywele ndefu sana. Alikuwa ni mwanamke mrembo lakini alitaka kuwa mrembo zaidi ya alivyokuwa. Lakini aliishia kutenda kosa kubwa sana. Kama Mungu ametupa mvi, ni lazima tuzikubali maana zinatoka kwa Mungu. Jambo hilo ni lazima litimie kwenye maisha yetu.
Nikasema: “Bwana, sikujua kuwa kubadili rangi ya nywele ni dhambi.” Kisha nikasema: “Bwana, msaidie. Mrehemu.”
Bwana alipeleka Mchungaji kwa mwanamke huyu wakati alipokuwa duniani. Alikuwa ni Mwinjilisti. Mwanamke huyu alikuwa akihubiri na kufundisha. Kama ilivyo kwa baadhi, pale wanapohubiri, wanajaribu kujionyesha wao kwanza kwenye kusanyiko ili wakubalike kwa jinsi walivyo, ili waweze kuhubiri na kufundisha kile wakitakacho.
Mwanamke huyu hakuwahi kutaka kuelewa makusudi ya Mungu. Hatimaye alikufa na sasa yuko kuzimu. Huyu alikuwa ni mwanamke aliyemtumikia Bwana.
Bwana akasema: “Binti yangu, naenda kukuonyesha wanawake wanaotumia vipodozi kwenye nyuso zao.”
Nikasema: “Bwana, hata mimi natumia vipodozi pia. Natumia poda kwenye uso wangu ili nionekane mrembo zaidi, ili kuziba mabakabaka kwenye uso wangu.”
Bwana akasema: “Vitu hivyo havinipendezi mimi. Nafurahishwa na mwonekano wa asili wa Watakatifu wangu. Mwanamke anatakiwa anifurahishe mimi na mume wake. Kwa hiyo, hahitaji vipodozi ili kuonekana mrembo kwa mtu mwingine yeyote.”
Wakati huo ndipo nilipomwona mwanamke ambaye alikuwa ameshikilia kioo mikononi mwake na mapepo yalikuwa yanamlazimisha kupaka vitu fulani usoni mwake. Alipaka majimaji fulani usoni kisha ngozi ya uso wake ikabanduka na kuanguka. 
Huenda unasoma ushuhuda huu na unasema kwamba vipodozi si dhambi. Nikwambie sasa – Mungu anaposema jambo, sote ni lazima tutii! Mwanamke yule alikosa kutii alipokuwa duniani. Alikuwa akitumia vipodozi hapa duniani na sasa yuko kuzimu. Kule analazimishwa kupodoa uso wake usiku na mchana.
Bwana akasema: “Vitu hivyo havinipendezi mimi. Unakumbuka niliposema kuwa yule atakayeupenda ulimwengu ni adui wa Mungu?”
Ni lazima tutii mstari huo wa kwenye Biblia: Msiipende duni, wala mambo yaliyoko katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. (1 Yohana 2:15).
Sote tutahukumiwa kwa neno hili. Aina zote za vipodozi unazotumia hapa duniani, utavitumia na kuzimu pia. Nilikuwa nikitumia “wet-lips” ili kufanya midomo yangu ing’ae na kuwafanya watu wengine wanione.
Nikasema: “Bwana, unisamehe maana nilikuwa na hatia ya jambo hili.”
Bwana akasema: “Ninafanya hivi kwa sababu ya upendo nilionao kwa roho yako. Ili kuleta hofu ya uzito wake ndani yako; ili uweze kuelewa uzito wa matokeo; ili kwamba uweze kuwaeleza na wengine waache kutumia vipodozi.”
Mwanamke yule alikuwa katikati ya moto huku akiendelea kulazimishwa kujipodoa uso wake. Matokeo yake uso wake na midomo yake vilikuwa vinadondoka chini.
Enyi wanawake wa Mungu; wanawake wa Mungu msiwatazame majirani zenu. Yatazamani maisha yenu binafsi leo na kumwomba Mungu. Sema: “Bwana, ni mambo gani ninayotenda ambayo hayakupendezi?” Muulize Bwana naye atakujibu. Mungu huwa anajibu.
KUNDI LA SABA LA ROHO NILILOONA KUZIMU: WANAWAKE WANAOVAA MAPAMBO YA VITO
Bwana aliniambia: “Sasa nitaenda kukuonyesha waliko wanawake wanaovaa mapambo ya vito.”
Hapo nilimwona mwanamke ambaye alikuwa akilazimishwa na mapepo kuvaa hereni kwenye masikio yake. Joka kubwa lilikuja kwake naye alivaa hereni masikioni mwake. Kisha lile joka lilijiviringisha kwenye shingo yake.
Bwana yuko kinyume kabisa na wanawake wanaotumia mapambo ya vito. Nikasema: “Bwana, lakini mbona hili ni pambo la kawaida tu?”
Bwana akasema: “Binti yangu, vitu hivyo havinipendezi Mimi.”  
KUNDI LA NANE LA ROHO NILILOONA KUZIMU: FAMILIA NA WAPENDWA
Bwana alinipeleka mahali ambako nilimwona mwanamke akilia; akipiga kelele sana kuzimu. Nilimwuliza Bwana: “Bwana, mwanamke huyu ni nani?” na Bwana akasema: “Nitakuonyesha huyu ni nani.”
Alikuwa ni mwanamke niliyemfahamu miaka mingi iliyopita. Tangu nilipoyatoa maisha yangu kwa Bwana, sikuwahi kuhubiri ujumbe wa wokovu kwa mwanamke huyu.
Bwana aliniambia: “Yuko hapa kuzimu kwa sababu yako. Nilitaka kuiokoa roho yake kupitia wewe lakini hukuwahi kwenda kumweleza habari zangu.”
Nikasema: “Bwana, naomba unihurumie!”
Mwanamke yule aliomba rehema kwa Bwana nami nikasema: “Bwana, mhurumie.”
Mwanamke huyu alikuwa mlevi wakati alipokuwa angali duniani. Bwana alimwonyesha kupitia skrini fursa zote alizokuwa nazo wakati angali duniani za kuyatoa maisha yake kwa Bwana lakini alikataa. Siku ambayo nilisukumwa kuongea na mwanamke huyu, sikusema naye kwa sababu aliniambia kuwa angeniua kama ningemweleza habari za Bwana. Niliogopa na sikuweza kumhubiria. Hivi sasa yuko kuzimu akiteseka. Jina lake ni Augustina.
KUNDI LA TISA LA ROHO NILILOONA KUZIMU: WATUMIA DAWA ZA KULEVYA
Nilimwona mwanamume ambaye alikuwa akilazimishwa na mapepo kutumia dawa za kulevya kuzimu. Alipewa kitu kama sigara ikiwa imejaa miali ya moto ili aivute. Nikasema:  “Bwana, mwanamume huyu ni nani?”
Bwana akaniambia: “Njoo umwone ni nani.”
Nilimkaribia na nikashangaa kuona kuwa kumbe ni kaka yangu Esau yuko kuzimu! Nilijawa na huzuni sana kumwona kaka yangu akiteseka kuzimu. Nikasema: “Bwana, mhurume kaka yangu.”
Kaka yangu alinyoosha mkono wake ukiwa umejaa miali ya moto na kuanza kumwomba Bwana rehema. Bwana akamwambia kaka yangu: “Mwanangu, unakumbuka kuwa uliyatoa maisha yako kwangu wakati ulipokuwa gerezani na ukaniomba nikutoe gerezani; na ukaahidi kwamba ungenitumikia katika maisha yako yote?”
Kaka yangu akasema: “Bwana najua; nakumbuka. Lakini tafadhali nisamehe. Nipe tu fursa ya kutoka mahali hapa.”
Bwana alimwonyesha skrini na tukaweza kuona wakati akiwa gerezani miaka mingi iliyopita. Bwana alimwonyesha siku hiyo pamoja na ahadi zote alizoahidi kumtumikia Bwana.
Bwana alimtoa gerezani kwa ili aweze kumtumikia lakini alipotoka, alikataa kutimiza ahadi yake ya kumtumikia Bwana. Na miaka miwili baadaye aliuawa mikononi mwa mama yangu. Kaka yangu alikufa kifo kibaya kwa sababu ya kutokutii kwake.
Huyu ni kaka yangu ambaye ninakuambia habari zake. Kaka yangu mwenyewe yuko kuzimu! Inatisha! Sikutaka kulisema hili waziwazi lakini Bwana aliniambia kuwa ni lazima niliseme. Nililia sana nilipomwona kaka yangu akiwa kuzimu.
Huwezi kupata picha jinsi Bwana wetu anavyolia kwa ajili ya roho zilizoko kuzimu, Bwana aliniambia.
Bwana alinionyesha mwanamke aliyekuwa Mchungaji wakati alipokuwa duniani. Alikuwa amekalia kiti kilichozungukwa na miali ya moto. Alikuwa anavalishwa wigi (nywele za bandia) kuzimu na jingine tena juu yake. 
Bwana aliniambia: “Alikuwa ni Mtakatifu wangu wakati fulani uliopita. Alikuwa ni Mchungaji wangu. Alikuwa ni mwanamke mkubwa wa Mungu. Nilimtumia kwa kiwango cha juu sana, lakini aliasi Neno langu.”
Nikasema, “Bwana, mhurumie.”
Alinyoosha mkono wake kwa Bwana kuomba msaada. Najua kuwa hadithi ya mwanamke huyu itasababisha maumivu makubwa sana ya kihisia.
Alikuwa ni mwanamke aliyemtumikia Bwana. Alibadili mafundisho ya Bwana. Alimwacha Bwana kwa ajili ya vitu vya dunia. Alikuwa akifanya vitu ambavyo vilikuwa havimpendezi Bwana. Alikuwa akisema maneno yasiyo na maana kila wakati. Bwana alimwonyesha kwenye skrini mambo yote aliyofanya wakati akiwa duniani.
Bwana alimwuliza: “Binti yangu, unaweza kukumbuka pale nilipokuletea Neno langu kupitia Mtakatifu wangu, Elma?”
Dada yangu, Elma alizungumza na mwanamke huyu wakati akiwa duniani lakini yeye alimtukana dada yangu. Alikataa kutii na Bwana akasema: “Hiyo ilikuwa ni fursa yako ya kurekebisha njia zako na kunirudia mimi lakini ulikataa na hii ndiyo adhabu yako. Je, unakumbuka jinsi ambavyo binti yako alikukumbatia na kusema, Mama rudi lakini hukutaka kusikiliza?”
Bwana alimgeuzia mgongo na mwanamke yule akaanza kutukana.
Bwana wetu Yesu Kristo alimgeuzia mgongo na kuanza kulia sana.
Nikauliza: “Bwana, kwa nini unalia?”
Bwana akasema: “Huwezi kujua jinsi ninavyojisikia kuona roho zikiwa hapa.”
NILIONA KITI CHA ENZI CHA SHETANI KUZIMU
Bwana aliniambia: “Naenda kukuonyesha kitu binti yangu. Sikuwa nimemwonyesha mtu yeyote kitu hiki kabla. Nataka ukione ili uweze kuelewa kuwa shetani ni mwongo. Shetani huiga mambo.”
Nikasema: “Bwana, tafadhali naomba unitoe mahali hapa. Siwezi tena kuvumilia zaidi.”
Bwana akanionyesha kiti cha enzi kuzimu. Niliona kiti cha enzi cha shetani kuzimu! Shetani anamwiga Mungu Mwenyezi huko kuzimu. Nilimwona akiwa amekaa kwenye hicho kiti chake cha enzi. Shetani ni mbaya sana. Naye anajifanya ana ngazi za madaraka.
Niliweza kuona malaika wamemzunguka lakini wote ni mapepo. Alikuwa amevaa joho jeupe likiwa limejaa madoadoa na ni chafu sana. Niliona wazee ishirini na wanne wakimwabudu shetani kuzimu. Walidondosha taji zao na kumwabudu. Niliweza kuona kuwa wote walikuwa ni mapepo.
Kiti cha enzi cha shetani kimejaa mambo yaliyoigwa kutoka Mbinguni. Kila kitu kilionekana kibaya sana.
Nikauliza: “Bwana, hii ni nini?”
Wakati huohuo, shetani aliita mojawapo ya mapepo yake na akalituma kwenda kumleta mtu fulani kutoka kuzimu. Mapepo yanafanya kila kitu ambacho shetani anayaambia yafanye. Kila wakati huwa anayatuma duniani ili kufanya uharibifu.
KITABU CHA KUZIMU
Bwana akasema: “Nataka ufahamu kuwa shetani huiga mambo ya mbinguni. Nataka ufahamu kuwa shetani ni halisi. Shetani anataka kuuharibu ulimwengu.”
Mahali pale niliweza kuliona pepo katika umbo la malaika wa kishetani likiwa na makucha marefu sana na limeshikilia kitabu mkononi mwake. Pepo hili lilikuwa linaandika kitabuni majina ya watu ambao wataenda motoni.
Nikauliza: “Bwana, kwa nini wanafanya hivi?”
Bwana akasema: “Nenda ukaiambie dunia kwamba watu wasio na Yesu Kristo maishani mwao, shetani ameshaandika majina yao kwenye kitabu cha kuzimu.”
Bwana akaniambia tena: “Angalia, pepo hili limetumwa kwenye barabara ili kusababisha ajali. Kuna ajali nyingi zinazotokea kwenye maeneo mbalimbali. Shetani na mapepo yake ndio wanaohusika na mambo haya.”
Nikasema: “Bwana, hali hii ni mbaya sana.”
Bwana akasema: “Ni muhimu uone mambo haya yote ili uwe na uwezo wa kuielezea dunia jinsi kuzimu kulivyo, ili dunia iweze kujua na kuamini kuwa kuzimu kweli kupo.”
NILITESWA NA BAADHI YA MAPEPO KUZIMU
Kisha Bwana alikuwa akinipeleka kwenye sehemu nyingine. Nikasema: “Niondoe mahali hapa. Hapa ni kubaya sana, tafadhali.”
Bwana alinishikilia mkono wakati tukiwa bado tunaenda. Ghafla lilitokea pepo la kutisha, kubwa lenye makucha marefu.
Pepo lile lilikamata nywele zangu na likaruka na mimi. Wakati huu sikuweza kumwona Bwana. Bwana alipotea na kuniacha peke yangu. Pepo lile lilinikokota hadi kwenye sehemu nyingine, kisha mapepo mengine yalikuja na kuanza kunitesa kwa namna mbalimbali.
Sauti ikawa inaongea kwenye ufahamu wangu ikisema: “Utabakia hapa kuzimu milele na utateswa, na utahisi maumivu na majonzi yote ambayo yako hapa kuzimu.”
Nikasema: “Bwana, siwezi kustahimili haya. Siwezi kustahimili haya!”
Pepo jingine lilikuja kwangu likiwa na mdomo mrefu sana, likapanda juu yangu. Nilijaribu kulisukuma lakini sikuweza. Liliingiza domo lake kwa nguvu kinywani mwangu  na nilihisi mate yake kwenye kinywa changu chote. Nikapiga kelele: “Bwana, kwa nini unaruhusu haya yote yanipate?”  
Bwana akasema: “Ni muhimu; ni muhimu kwa wewe kuwaambia watu duniani jinsi kuzimu kulivyo hasa ili waweze kuelewa makusudi.”
Bwana akasema: “MIMI NI MUNGU MTAKATIFU, wako watu kanisani ambao wanafanya kila aina ya mambo machafu kwa vinywa vyao.”
Nikauliza: “Bwana, nitawezaje kusema mambo haya yote?”
Bwana akaniambia: “Sema kila kitu nilichokuonyesha.”
Bwana alinionyesha skrini na nikaweza kuona uchafu mwingi. Wako watu wengi kanisani leo ambao wanatenda aina mbalimbali za dhambi za siri.
Nikauliza: “Bwana, hii ni nini?”
Bwana akasema: “Waambie wabadilike. Waambie kuwa MIMI NI MUNGU MTAKATIFU. Waambie kuwa vinywa vyao ni kwa ajili ya kunitukuza mimi na si kwa ajili ya uchafu.”
Nikasema: “Bwana, ondoa pepo hili mwilini mwangu” maana lile pepo lilikuwa linanyonya mwili wangu wote. Mate yake yalikuwa meusi sana na yamefunika mwili wangu wote. Hali ilikuwa inatisha. Harufu ya kuzimu ni mbaya mno kuliko hata mbwa aliyeoza. Sina maneno ya kuweza kuielezea. Nikasema: “Bwana, nisaidie. Siwezi kustahimili zaidi.”
Bwana akaniambia: “Binti yangu, tulia. Ni muhimu sana kwa wewe kupitia mambo yote haya.”
Nikauliza: “Bwana, kwa nini uliniacha peke yangu?”
Mara pepo jingine lilikuja. Likanichukua hadi kwenye sehemu nyingine. Kule niliona roho zingine zikicheza. Nikauliza: “Bwana, nini kinachofuata cha mimi kufanya sasa?”
Niliwekwa ili nicheze katikati ya moto. Kulikuwa na vitu humo ndani vikinilazimisha kucheza. Nikauliza: “Bwana, kwa nini haya yananipata?”
Bwana akasema: “Kwa sababu wewe ni mchezaji. Huwa unacheza unaposikia kila muziki wa Kikristo na miziki mingine inayokupendeza wewe.”
Bwana akaniambia tena: “Mambo hayo hayanipendezi mimi.”
Nikasema: “Bwana, nisamehe. Sitarudia tena.”
Bwana akasema: “Kama ulivyo wewe, wako watu wengi miongoni mwa watu wangu ambao hucheza kama watu wa dunia. Wanachezesha viuno vyao kama watu wa kidunia. Mambo hayo hayanipendezi mimi.”
Nikasema: “Bwana, nisamehe. Naomba unihurumie,” kwa sababu roho yangu ilikuwa inaungua. Nilikuwa katikati ya miali ya moto. Ninaweza kukuambia jinsi kuzimu kunavyotisha kwa sababu roho yangu ilikuwa pale. Sisemi uongo hata kidogo. Nawaambia kweli tupu. Kuzimu ni halisi! Nilikuwa pale!!
Mapepo yalinitoa mahali pale na kunipeleka sehemu nyingine tena. Kulikuwa na minyoo mingi sana hapo. Minyoo ile iliingia sehemu mbalimbali za mwili wangu – kupitia masikioni, machoni.
Nikasema: “Bwana, tafadhali nihurumie. Nitafanya kila ulichoniambia nifanye, lakini tafadhali naomba unitoe hapa.”
Bwana akasema: “Hii ni muhimu sana ili kila mtu aweze kuelewa kuwa kuzimu ni mahali halisi. Watu wengi husema kuwa kuzimu hakupo. Nenda ukawaambie kuwa kuzimu kupo.”
Palepale nilikumbuka kitabu cha Luka 16:19-31 kinachoongelea juu ya tajiri na Lazaro. Pale kaka yangu aliponyoosha mkono alisema: “Bwana, peleka ujumbe huu kwa familia yangu ili wasije kuja huku kuzimu.”
Bwana aliniambia: “Kumbuka hadithi ya Tajiri na Lazaro. Tajiri alipoomba kwamba Lazaro atumwe duniani kuiambia familia ya tajiri kwamba kuzimu kweli kupo.”
Niliondolewa kwenye sehemu ambako nilikuwa nateswa na minyoo. Bwana akaniambia: “Ni muhimu sana ukaseme mambo yote uliyoona ili roho ziokolewe. Ninafanya yote haya kwa sababu ya upendo nilio nao kwa wanadamu. Kama  nisingekuleta hapa, ningekupoteza.”
Bwana akasema tena: “Roho nyingi zitaokolewa kutokana na ushuhuda huu.”
Nikasema: “Tafadhali Bwana. Niondoe huku kuzimu. Siwezi kuendelea kuwa hapa!”
Nilipitia mateso mengi sana kuzimu huku moto ukiwa umefunika mwili wangu wote.
Hatimaye, ghafla nuru kali ilitokea na Bwana akanitokea. Nilimkimbilia Bwana na kumkumbatia. Nikauliza: “Bwana, kwa nini uliniacha peke yangu? Kwa nini uliniacha peke yangu? Kwa nini???”
Bwana akasema: “Ndiyo binti yangu. Binti, ilikuwa ni muhimu sana uone maumivu ambayo roho zinayapata hapa kuzimu ili uwe na uwezo wa kuuelezea ulimwengu uliobakia.”
Kisha Bwana alinitoa pale. Bwana alinionyesha vitu vingine ambavyo sitaweza kuvisema kwa sasa. Mungu ataniambia ni lini niviseme vitu hivyo. Hivi sasa nitakueleza tu vitu vile ambavyo Bwana aliniambia niviseme.
SAFARI YANGU YA PILI KWENDA MBINGUNI – KILA KITU KIKO TAYARI MBINGUNI
Bwana akasema: “Nitakuonyesha mahali ambako niliwaambia mitume wangu kwamba naenda kuwaandalia mahali, ili mimi niliko na wao watakuwa hapo pia, ili ukamwambie kila mtu kwamba mambo haya ni halisi.”
Bwana alikuwa ananipeleka moja kwa moja hadi mbinguni. Kisha niliona mlango mkubwa ukiwa wazi.
Nikasema: “Bwana, kuzimu ni kubaya sana. Lakini mahali hapa [mbinguni] ni kuzuri.”
Bwana akaniambia: “Binti yangu, nitakuonyesha Mbinguni.”
Na niliona sehemu kama jiji kubwa mbinguni. Ndiyo, napaita mahali pale jiji kubwa kwa sababu hicho ndicho hasa nilichoona. Bwana alinipeleka kwenye mtaa mmoja mbinguni. Mitaa ya mbinguni ni ya dhahabu tupu. Ni dhahabu halisi kabisa! Niliona maua mazuri  pembeni ya mitaa ya mbinguni. Ni maua mazuri mno kiasi kwamba hakuna maua hapa duniani yanayoweza kulinganishwa nayo!
Bwana alinipeleka mahali fulani na akaniambia: “Ninaenda kukuonyesha mto. Nitakuingiza humo.”
Kulikuwa na mawemawe kwenye mto huo. Mto wenyewe ni kama kioo. Mawe ya kwenye mto ule yanang’aa. Kulikuwa na samaki kwenye mto huo pia. Bwana alimtoa samaki mmoja kwenye mto ule na kumshika mkononi; na samaki yule alikuwa na furaha, huku akichezacheza mikononi mwa Bwana.
Nikasema: “Bwana, mrudishe samaki majini, atakufa.”
Bwana akasema: “Hakuna anayekufa hapa. Mauti haipo hapa. Mahali hapa kumejaa uzima tu. Kila kitu hapa ni uzima.”
Nikasema: “Bwana, kuna watu wengi sana kule wanaoteswa. Kwa nini hukuwapatia fursa ya kurekebisha njia zao ili waje hapa Mbinguni?”
Bwana akasema: “Wako pale kutokana na uasi wao.”
Bwana alinichukua kama mtoto mdogo kutoka kwenye mto hadi mahali pengine. Mto huo ni mzuri sana. Kila kitu kinachotungoja Mbinguni ni kizuri sana!
Kisha niliomba jambo kwa Bwana. Nilimwambia Bwana: “Ziko wapi roho ulizoziokoa? Wako wapi hapa mbinguni?”
Bwana akasema: “Nitakuonyesha.”
Bwana alinipeleka mahali ambako alinionyesha mmojawapo wa dada zangu katika Kristo ambaye alishakufa. Jina lake ni Aurora Esperanza. Bwana alinionyesha dada mwingine. Alikuwa ni binti wa mmoja wa dada zangu, dada Grace. Alionekana akiwa mdogo na mzuri sana.
Bwana akasema: “HAWA NI WATAKATIFU WANGU.”
Ana amani sana Mbinguni. Watakatifu walioko Mbinguni ni kama malaika. Niliwaona Watakatifu wachanga Mbinguni. Mavazi yao ni tofauti. Mahali ambako Bwana alinionyesha pamejaa maua mazuri. Ni mahali pazuri sana penye harufu nzuri sana. Nilikuwa Mbinguni! Nilipaona Mbinguni! Nilipagusa Mbinguni!
Bwana aliniambia: “Sasa nitakuonyesha yaliko mavazi ya Watakatifu wangu.”
Nikamwuliza Bwana: “Je, utanionyesha vazi langu?”
Bwana akasema: “Nitakuonyesha mavazi ya Watakatifu Wangu.”
Bwana alionyesha baadhi ya mavazi, mavazi meupe ambayo yamepambwa kwa dhahabu. Mavazi hayo yana mikanda ya dhahabu na yote yameandikwa majina juu yake. Bwana alinionyesha pia mavazi mengine. Mavazi haya ni ya baadhi ya watu ambao bado wako duniani ambao bado hawajampokea Bwana wetu Yesu Kristo.
Bwana akaniambia: “Haya ndiyo mavazi ya Watakatifu Wangu na haya ndiyo mavazi ya watu wengine ambao bado wako duniani, ambao bado hawajanipokea mimi.”  
Nikasema: “Bwana, nataka kuona mataji. Nataka unionyeshe taji ya Mchungaji wangu, na taji yangu mwenyewe. Bwana, nataka kuona taji yangu.”
Bwana akasema: “Nitakuonyesha.” Bwana alinionyesha mataji hayo, ni mazuri sana. Nitakueleza juu ya taji ya Mchungaji wangu. Nilimwomba Bwana anionyeshe taji yake maana nilitaka kumletea Mchungaji wangu habari njema.
Bwana alinionyesha taji yangu. Taji yangu haikuwa na vito. Haikuwa kama taji zingine ambazo zilinivutia sana kama ile ya Mchungaji wangu.
Nikamwuliza Bwana: “Kwa nini taji yangu haina vito?”
Bwana akasema: “Huwezi kuelewa mambo aliyopitia hadi kufikia kuwa na taji yenye vito vingi kama hii.”
Malaika alichaguliwa kuweka mataji na pia vito kwenye mataji. Watu wanapotubu na kuja kwa Yesu Kristo, unapoleta roho kwenye Ufalme wa Mbinguni, malaika ataweka kito kwenye taji yako. Unapowasaidia wenye shida, malaika ataongeza  kito kingine kwenye taji yako. Unapowasaidia maskini na wasio na mahali pa kuishi, malaika ataongeza  vito zaidi kwenye taji yako.
Bwana alikuwa anaongea nami kuhusu Mchungaji wangu. Alisema kuwa ameshateseka sana kwa ajili ya Ufalme wa Mungu; na kwamba alipitia magumu mengi hadi kupata taji kama hiyo. Ana moyo sana wa kuleta roho za watu kwa Kristo.
Bwana akasema: “Mwambie ashikilie kwa nguvu kile alicho nacho ili mtu mwingine asije akachukua taji yake.”
Nilimweleza Mchungaji wangu yale yote ambayo Bwana aliniambia.
Halafu Bwana alinionyesha mataji ya Watakatifu Wake wote.
Alinionyesha mataji ya watu ambao hawajayatoa maisha yao kwake lakini bado wako duniani.
NILIONA KITI CHA ENZI CHA MUNGU MBINGUNI
Bwana alisema: “Binti yangu, nitakuonyesha kitu.”
Kutokea mbali, niliona kiti cha enzi kikubwa sana; cha thamani sana.
Bwana akasema: “Hiki ni kiti cha enzi cha Baba yangu.”
Bwana alikuwa amekaa pale. Nuru kali ya kiti cha enzi ilinifanya nisiweze kuona mengi. Niliona baadhi ya wazee wakitupa taji zao chini na kuinama ili kumwabudu Bwana. Hawaachi kumwabudu Bwana Mbinguni.
Niliona malaika wengi sana wakiwa wamesimama kuzunguka kiti cha enzi cha Mungu. Kitabu cha Ufunuo kinaongelea kuhusu sehemu hii. Mbingu ni halisi. Niliona mbingu kwa sababu nilifika pale.
Bwana akasema: “Binti, kaiambie dunia kwamba mbingu ni halisi. Zungumza binti yangu.”
Nikauliza: “Bwana, unadhani wataniamini?”  
Bwana akasema: “NDIYO.”
Nilikuwa nazungumza na Bwana kama ambavyo naweza kuzungumza na kaka yangu au na Mchungaji wangu.
Niliona malaika wengi sana Mbinguni; na kila walipomwona Bwana, walivua mataji yao na kuinama na kumwabudu Bwana. Nilijawa na furaha sana kuona mambo haya. 
Bwana akasema: “Binti yangu, UTUKUFU WOTE NI MALI YANGU. UTUKUFU WOTE NI WANGU.”            
Hapa nilielewa kwamba Mungu hashirikiani utukufu wake na yeyote. Malaika walikuwa wakiimba, wakimwabudu Bwana muda wote. Hawaachi hata kidogo kumwabudu Bwana. Niliona jinsi kanisa lenye wachungaji wazuri linavyomwabudu Bwana. Dada yangu, Yasmine, alikuwa akiwaongoza.
Bwana akasema: “Waambie kwaya ya kanisa la wachungaji wazuri waniabudu Mimi na waache kufanya mambo yasiyonipendeza. Waambie kuwa kila wanaponiabudu, malaika Mbinguni huabudu pamoja nao.”
Ujumbe huu ni kwa wote wanaoabudu. Bwana anataka mmwabudu zaidi.
“Waambie waniabudu Mimi,” Bwana alisema.
Malaika walikuwa wakipiga vyombo mbalimbali katika kumwabudu Bwana.
MUNGU WETU NI BABA MTAKATIFU, AMINA
Malaika ni wazuri sana. Wanapomwabudu Bwana. Niliona amani kubwa sana kati yao. Waliabudu kutoka moyoni.
Bwana alinipeleka sehemu nyingine. Niliwaona malaika saba wameshikilia tarumbeta saba. Na karibu yao, kulikuwa na malaika wengine saba wameshikilia vikombe mikononi mwao. Walikuwa ni malaika wakubwa na warefu sana. Walivaa mavazi meupe sana; weupe ambao hata hauelezeki!
Nikauliza: “Bwana, malaika hawa ni akina nani?”
Bwana akasema: “Malaika hawa wanasubiri kutumwa duniani ili kuiharibu dunia.”
Malaika wale tayari wana tarumbeta mikononi mwao. Wanasubiri tu Bwana awaambie waanze kuzipiga.
Nikauliza: “Bwana, mbona ni warefu hivyo?”
Bwana akasema: “Kwa kuwa wao ni wana wa Mfalme.”
Nilikuwa nimekusudia kuuliza maswali zaidi. Lakini Bwana akaniambia: “Usiwe mdadisi sana. Usiulizeulize maswali mengi mno. Wewe onyesha tu yale ambayo nimekuonyesha; mambo ambayo nimekwambia useme. Waambie kuwa kuna Mbingu moja tu na wala hakuna nyingine. Waambie kuwa Mimi ni halisi, maana watu wengi hawazungumzi kuhusiana na Mimi. Waambie kuwa Mungu yuko pale juu akiwangoja.” 
Kisha Bwana akasema: “Sasa nitakuonyesha kile kinachoendelea miongoni mwa watu wangu.”
Bwana alinionyesha sehemu moja. Sehemu ile ilikuwa na pazia. Halafu akasema: “Ona kile kinachoendelea kwenye Kanisa langu. Ndani ya Kanisa langu yapo mambo mengi ambayo hayanipendezi. Nitaleta kwa Baba yangu taifa Takatifu tu. Kanisa langu haliko tayari. Nenda kawaambie wajiweke tayari kwa sababu tarumbeta karibu italia.”
NILIONA MEZA YA BWANA IMESHAANDALIWA TAYARI
Bwana akasema: “Sasa nitakuonyesha mahali ambako Watakatifu wangu watakula pamoja na Mimi.”
Akanionyesha meza kubwa sana, imepambwa vizuri kwa vitambaa vyeupe, vikombe vya dhahabu, huku kukiwa na viti kila mahali, na viti vyote vina majina ya Watakatifu yameandikwa juu yake. Sikuweza kuelewa majina yale. Nilimwomba Bwana anionyeshe kiti changu.
Bwana alinionyesha kiti changu na kusema: “Liambie Kanisa langu lijiandae. Waambie watu wangu kwamba meza imeshaandaliwa.”  
Nikasema: “Bwana, hapa ni pazuri sana.” Nilitaka kukaa kwenye kiti kimojawapo.
Bwana akasema: “Usikae kwenye kiti. Bado muda haujafika.”
Kisha niliona malaika wakienda na kurudi, na mmoja wao alikuja na kuzungumza na Bwana moja kwa moja masikioni mwake. 
Nikamwuliza Bwana: “Amesema nini?”
Bwana akasema: “Usiwe mdadisi sana.”
Kisha malaika alikuja tena na kuzungumza masikioni mwa Bwana. Bwana akasema: “Binti yangu, muda umeshafika wa wewe kurudi. Kaliambie Kanisa langu wajiandae. Kawaambie kila kitu nilichokuonyesha.”
Nikasema: “Bwana, hapanaaaa! Sitaki kurudi.”
Bwana akasema: “Ndiyo, ni lazima urudi ukawaambie kila kitu ulichoona. Waambie kuwa meza iko tayari, inawangoja. Ni lazima mjiweke tayari.”
Wakati tukiwa tunaondoka, Bwana akasema: “Kanisa langu liko namna hii: baadhi ya watu ni wa nia mbilimbili, baadhi ni wanafiki, wengine hawako tayari, wengine hawanipendi Mimi kwa moyo wote, baadhi wanafanya mambo kwenye nyumba yangu kwa sababu wanalazimika tu kufanya, wengine wanataka waonwe na kusifiwa na wachungaji wao.”
Bwana alianza kulia!
WATOTO WASIO WATII, WANAOPOKEA SIMU WAKIWA KANISANI
Bwana alinionyesha Kanisa. Nilimwona mhubiri akihubiri madhabahuni na ghafla simu yake iliita. Mhubiri huyu aliacha kuhubiri. Alitoka nje ili kwenda kusikiliza simu yake.
Bwana akasema: “Unaona jinsi wanavyopuuza uwepo wangu; ona jinsi wanavyopuuza uwepo wangu. Mtu anapohubiri, anakuwa anahubiri Neno langu. Wanaona bora kwenda kusikiliza simu kuliko kushughulika na Mimi.”
Kisha Bwana akaniambia: “Sema, sema na Wachungaji waachane na mafundisho yao. Wanaweza kukuchukia kama wakitaka, lakini watu wengi wataelewa makusudi ya Mimi kukuleta hapa na wengi watatubu.” 
Ujumbe kwenu wachungaji. Watu wanaweza kuwachukia pale mnapoamua kuyafanya mapenzi ya Mungu. Haijalishi kama watawachukia. Sahauni mafundisho yenu wenyewe. Fuateni kile ambacho Mungu amewapa. Msijaribu kumfurahisha kila mtu. Msikubali kuridhia mambo asiyopenda Mungu.
Bwana akasema: “Nitaenda kuliunganisha Kanisa langu pamoja. Mimi nina Kanisa moja tu. Sina Kanisa jingine duniani zaidi ya Kanisa moja tu. Hili ndilo Kanisa nitakalolipeleka mbinguni. Hili ndilo Kanisa nitakalolikabidhi kwa Baba yangu.”
Sisi tulio wa Huduma ya Kiinjilisti ndio Kanisa la Mungu. Wale ambao wameyatoa maisha yao yote kwa Yesu Kristo. Wale ambao hawatendi dhambi tena. Wale ambao wameziacha njia zao za zamani ili kuyafanya mapenzi ya Mungu. Wale waliozaliwa upya. Hawa ndio watu watakaouona uso wa Mungu.
HITIMISHO
Ushuhuda wangu unakaribia mwishoni. Nimewaeleza kila kitu ambacho Bwana aliniambia niseme, kwa utukufu wa Mungu. Utukufu wote, utukufu wote ni wa Mungu.
Niko hapa kwa rehema za Mungu. Ni kwa rehema za Mungu tu ninawaambia mambo haya ambayo Bwana alinitaka niyaseme. Ujumbe huu utakwenda moyoni mwako na kubadili maisha yako ili kwamba uweze kutubu.
Mwulize Bwana: “Bwana, ni eneo gani la maisha yangu ambako ninashindwa?” Bwana atakujibu.
Napenda kukuambia kwamba Yesu Kristo anakupenda wewe; Yesu Kristo anakupenda wewe! Anataka kuyabadili maisha yako. Yesu Kristo hataki uende jehanamu bali anataka uende Mbinguni. Mbingu ni halisi, na kuzimu nako ni halisi pia. Tubu sasa na uyatoe maisha yako kwa Yesu Kristo. Wokovu unapatikana kwa Yesu Kristo tu!
Yesu Kristo anagonga kwenye mlango wa moyo wako kupitia ujumbe huu. Mtafute Bwana kwa moyo wako wote, naye atafanya mambo makubwa kupitia wewe.
Bwana akasema: “Mambo yote haya niliyokuonyesha yalishatabiriwa kwenye Kitabu cha Ezekieli, Kitabu cha Danieli na Kitabu cha Ufunuo. Mafunuo yote haya yamo kwenye Biblia.”
Ninaomba kwamba ushuhuda huu ukabadilishe maisha yako kwa ajili ya utukufu wa Mungu. AMINA.
MUNGU awabariki nyote.
**********
Ushuhuda huu nimeutafsiri kutoka kwenye toleo lake la Kiingereza ambalo linaweza kupatikana kwa kubofya kwenye kiungo kifuatacho: http://www.divinerevelations.info/Adelaida/index.htm